Pata taarifa kuu
UFARANSA-ICC

Ufaransa yazisihi Burundi, Afrika Kusini na Gambia kutojiondoa ICC

Ufaransa imeziomba nchi tatu zilizotangaza uamuzi wao wa kujiondoa kutoka Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC), ambayo wanaishtumu hasa kuzilenga nchi za Afrika pekee, kurejelea "upya" uamuzi wao, Wizara ya Mambo ya Kigeni ya Ufaransa imesema.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa, Jean-Marc Ayrault akisem akushangazwa na uamuzi wa Burundi, Afrika Kusini na Gambia wa kujiondoa ICC..
Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa, Jean-Marc Ayrault akisem akushangazwa na uamuzi wa Burundi, Afrika Kusini na Gambia wa kujiondoa ICC.. Emmanuel Makundi/RFI
Matangazo ya kibiashara

"Tunaziomba nchi tatu zilizochukua uamuzi huo kufikiria upya nia yao na tuendelea kuweka mbele mazungumzo yenye kujenga kuhusu utendaji wa mfumo wa mahakama ya kimataifa ya makosa ya jinai, " ilisema Wizara ya Mambo ya Nje Jumatatu Oktoba 31 katika taarifa yake.

"Mapambano dhidi ya ukatili ni muhimu kwa heshima ya haki za binadamu, maridhiano na amani ya kudumu," Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa Jean- Marc Ayrault, akiongeza kuwa "mahakama ya kimataifa katika suala hili ina jukumu la kipekee kama mahakama moja pekee ya jinai yenye kudumu na yenye uwezo wa kushughulikia kesi kwa wote. "

Oktoba 18, Burundi ilitangaza rasmi kuwa inajiondoa kutoka ICC, ikifuatiwa Siku chache baadaye Oktoba 21 na Afrika Kusini, baada ya utata uliyosababishwa na kukataa kumkamata Rais wa Sudan Omar al-Bashir, anayetafutwa na ICC kwa mauaji ya kimbari, uhalifu dhidi ya ubinadamu na uhalifu wa kivita huko Darfur.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.