Pata taarifa kuu
ICC-BOTSWANA-AFRIKA KUSINI

Botswana na Afrika Kusini katika mzozo kuhusu Afrika kujitoa ICC

Mvutano mkubwa huenda ukaibuka kati ya nchi ya Afrika Kusini na Botswana, kuhusu nchi za Afrika kuendelea kujiondoa kwenye mkataba wa kimataifa wa Roma, ulionazisha mahakama ya kimataifa ya ICC.

Jengo la mahakama ya kimataifa ya makosa ya jinai, ICC.
Jengo la mahakama ya kimataifa ya makosa ya jinai, ICC. REUTERS/Jerry Lampen/File Photo
Matangazo ya kibiashara

Siku moja baada ya waziri wa sheria wa Afrika Kusini, Michael Masutha, kutangaza kuwa nchi yake imeshaandika barua umoja wa Mataifa kuwa haitakuwa tena mwanachama wa mkataba wa Roma ulioanzisha mahakama ya ICC, nchi ya Botswana imeuelezea uamuzi wa Afrika Kusini kama uamuzi wa "Kushangaza na majuto."

Kwenye taarifa yake, Botswana imesema kuwa haitajihusisha na nchi ambazo zinapiga kampeni nchi nyingine za Afrika kujiondoa kwenye mahakama ya ICC.

Waziri wa mambo ya nje wa Afrika Kusini, Maite Nkoana-Mashabane.
Waziri wa mambo ya nje wa Afrika Kusini, Maite Nkoana-Mashabane. http://www.russianembassy.org.za

Nchi ya Botswana inasema kuwa, nchi hizi kujiondoa kwenye mkataba wa Roma ulioanzisha mahakama ya ICC, ni sawa na kuwasaliti wahanga wa vitendo mauaji, kupata haki yao na kwamba ni kutaka kuwalinda wahalifu.

Botswana imeitaka nchi ya Afrika Kusini badala ya kujiondoa, iwasilishe malalamiko yake kuhusu mkataba wa Roma ulioanzisha mahakama hiyo, wakati wa mkutano wa nchi wanachama wa mahakama hiyo wiki ijayo.

Kufuatia matamshi hayo, waziri wa ushirikiano wa kimataifa wa Afrika Kusini, Maite Nkoana-Mashabane, amekosoa matamshi ya Botswana, akisisitiza kuwa Afrika Kusini inao wajibu na haki ya kujiamulia masuala yake ya ndani kwakuwa ni taifa huru.

Waziri wa mambo ya nje wa Botswana, Pelomoni Venson-Moitoi.
Waziri wa mambo ya nje wa Botswana, Pelomoni Venson-Moitoi. BOTSWANA Department of Foreign Affairs/Handout

Uamuzi wa Afrika Kusini kujitoa kwenye mahakama ya ICC, umekuja baada ya ule wa Serikali ya Burundi ambapo pia nchi ya Gambia nayo imeridhia kujitoa kwenye mahakama hiyo na kutoa taarifa kwenye umoja wa Mataifa wakiituhumu mahakama hiyo kwakuwa na upendeleo.

Msimamo huu wa Botswana unakuja wakati huu nchi za Afrika zikijiandaa kuchagua mkuu mpya wa tume ya umoja wa Afrika mwezi January mwakani, huku waziri wa mambo ya nje wa Botswana, Pelomoni Venson-Moitoi akiwa miongoni mwa wagombea na anayetaka nchi hizo zisalie kwenye mahakama hiyo.

Afrika Kusini sasa imeonesha wazi kuwa haina nafasi yoyote ya kumuunga mkono Venson kuwania kiti hicho kutokana na msimamo wake wa kutaka waendelee kuitambua mahakama ya ICC.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.