Pata taarifa kuu

Ramaphosa: Mkutano wa kilele wa BRICS utafanyika nchini Afrika Kusini Putin akiwepo au la

Mkutano wa kilele wa BRICS utafanyika nchini Afrika Kusini. Rais Cyril Ramaphosa amethibitisha hilo, huku baadhi ya vyombo vya habari vikizungumzia kuhusu kiongozi huyo akijaribu kutafuta njia nyingine ya Urusi kushiriki mkutano huo. Wakuu wa nchi za kundi hilo kutoka Brazil, Urusi, India, China na Afrika Kusini wanatarajiwa kukutana mjini Johannesburg kuanzia Agosti 22 hadi 24. Uwepo wa Vladimir Putin bado haujathibitishwa.

Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa, Juni 16, 2023.
Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa, Juni 16, 2023. REUTERS - VALENTYN OGIRENKO
Matangazo ya kibiashara

Na mwanahabari wetu mjini Johannesburg, Romain Chanson

Rais wa Urusi analengwa na waranti wa kukamatwa uliyotolewa na Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) na Pretoria, ambayo imetia saini Mkataba wa Roma, italazimika kumkamata. Licha ya kikwazo hiki, Afrika Kusini inang'ang'ania mkutano wake wa kilele ufanyike nchini humo.

Putin awepo au la, mkutano wa BRICS utafanyika ana kwa ana. Rais Cyril Ramaphosa anataka wakuu wa nchi waweze kuzungumza macho kwa macho, mara ya kwanza tangu mwaka 2019.

Viongozi 60 wa nchi wamealikwa, ikiwa ni pamoja na viongozi wote wa bara la Afrika, kwa sababu Cyril Ramaphosa anataka kufanya mkutano huu wa kilele wa muungano wa familia. Washiriki wana mwezi na nusu kuthibitisha kuhudhuria kwao katika mkutano huo.

Vladimir Putin anaonekana kutaka kusubiri hadi dakika ya mwisho kueleea nia yake. Kwa upande wake, Cyril Ramaphosa bado hajafichua mahitimisho ya kamati ya mawaziri inayohusika na kuchunguza uwezekano wa ziara ya rais wa Urusi licha ya Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu kutoa waranti ya kukamatwa kwa Vladimiri Putin.

"Putin anahofia zaidi usalama wake ikiwa ataondoka Moscow kuliko kukamatwa na ICC," anabaini mchambuzi wa masuala ya sayansi wa siasa Sanusha Naidu. Kuna uwezekano rais wa Urusi asihudhurii mkutano huu, anasema mchambuzi huyo wa mauala ya sayansi.

Putin anaweza kuwakilishwa na waziri wake wa mambo ya nje. Sergei Lavrov tayari amezuru Afrika Kusini mara mbili mwaka huu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.