Pata taarifa kuu

Upanuzi wa muda wa makubaliano ya nafaka: Mazungumzo ya simu kati ya Ramaphosa na Putin

Mwezi mmoja baada ya ujumbe wa amani nchini Ukraine na Urusi ulioongozwa na wakuu kadhaa wa nchi za Afrika, Rais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa, mmoja wa washiriki, amezungumza na mwenzake Vladimir Putin kwa simu Jumamosi hii Julai 15. Wawili hao wamejadili hasa mustakabali wa makubaliano ya nafaka katika Bahari Nyeusi, makubaliano ambayo yanaruhusu Ukraine kusafirisha ngano yake kutoka bandari zake, licha ya vita, na ambayo muda wake utamalizika Jumatatu Julai 17 jioni.

Rais wa Urusi Vladimir Putin na mwenzake wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa, hapa ilikuwa mwezi Oktoba 2019, huko Sochi.
Rais wa Urusi Vladimir Putin na mwenzake wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa, hapa ilikuwa mwezi Oktoba 2019, huko Sochi. AP - Sergei Chirikov
Matangazo ya kibiashara

Na mwanahabari wetu mjini Johannesburg, Claire Bargelès

Kulingana na Kremlin, Vladimir Putin amemkumbusha mpatanishi wake rais wa Afrika Kusini kwamba maombi ya Urusi ya kuondoa vikwazo kwa mauzo yake ya mbolea na bidhaa za chakula hadi sasa hayajaheshimiwa.

Mazungumzo haya yanakuja baada ya taarifa za rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan, ambaye alisema Ijumaa kuwa mwenzake wa Urusi "anakubali" kuendeleza eneo salama la kupitisha nafaka katika Bahari Nyeusi.

Cyril Ramaphosa anatarajia kuendeleza majadiliano, pia na Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky, ambaye tayari alikuwa alizungumza naye wiki hii, pamoja na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres.

Ikiwa makubaliano haya hayatarefushwa tena, Afrika hasa inaweza kukabiliwa na hali ngumu na kuona usalama wake wa chakula ukiwekwa katika hatari zaidi.

Marais wa Afrika Kusini na Urusi pia wamejadili mkutano wa kilele wa BRICS (Brazil, Urusi, India, China na Afrika Kusini), utakaofanyika mwishoni mwa mwezi Agosti huko Johannesburg, bila kutajwa kwa sasa ikiwa Vladimir Putin atashiriki au la mkutano huo: ushawishi wa hati ya kukamatwa kutoka Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu, anapaswa kukamatwa ikiwa atakanyaga ardhi ya Afrika Kusini, nchi hiyo ikiwa imetia saini Mkataba wa Roma.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.