Pata taarifa kuu

Ajali ya boti yasababisha vifo vya zaidi ya watu 100 nchini Nigeria

NAIROBI – Mamlaka nchini Nigeria zimesema watu zaidi ya 103 wamefariki baada ya boti lao kuzama katika jimbo la Kwara kaskazini mwa taifa hilo.

Watu zaidi ya mia moja wamefariki baada ya boti lao kuzama nchini Nigeria
Watu zaidi ya mia moja wamefariki baada ya boti lao kuzama nchini Nigeria CIA
Matangazo ya kibiashara

Msemaji wa Polisi katika jimbo hilo Okasanmi Ajayi amesema watu waliofariki ni família zilizokuwa zikitoka katika hafla ya harusi, na kwamba shughuli ya kutafuta miili zaidi inaendelea huku watu wengine 100 wakiokolewa.

Visa vya ajali za boti kuzama nchini Nigeria vimekuwa vikiripotiwa mara kwa mara, kutokana na kubeba uzani wa juu, ukosefu wa njia nzuri za kuzuia ajali na hali mbaya ya hali ya hewa.

Mwezi uliopita watoto 15 walizama na watu 25 kukosa kupatikana baada ya ajali ya boti kutokea katika jimbo la sokoto wakati wakirejea nyumbani wakitoka kuteka kuni.

Kutokana na utekeaji nyara unaotekelezwa na makundi ya watu wenye silaha na hali mbaya ya barabara , raia wa taifa hilo wamekuwa wakitumia sana usafiri wa boti, na juhudi za mamlaka ya maji nchini humo kupiga mafuruku usafiri wa boti nyakati za usiku ili kuzuia ajali, zimegonga mwamba.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.