Pata taarifa kuu

Rais Buhari ameahirisha zoezi la sensa ya watu na makazi nchini Nigeria

NAIROBI – Zoezi la kuhesabu watu nchini Nigeria, lililotarajiwa kufanyika kati ya Mei 3 hadi 7 mwaka huu, limeahirishwa.

Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari.
Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari. REUTERS - GONZALO FUENTES
Matangazo ya kibiashara

Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari ameidhinisha kuahirishwa kwa shughuli hiyo na kusema tarehe mpya itatangazwa na serikali mpya inayoingia madarakani itakayoongozwa na Bola Tinubu.

Buhari ametoa idhini hiyo Ijumaa Aprili 28, baada ya mkutano na baadhi ya wanachama wa baraza la serikali pamoja na tume ya kitaifa ya sensa ya watu na makazi, katika majengo ya rais huko Abuja.

Siku ya Jumamosi, waziri wa habari na utamaduni Alhaji Mohammad, amesema kwenye taarifa kuwa mkutano huo licha ya kuafikia maamuzi ya kuahirisha zoezi hilo, kuna umuhimu wa kufanyika, kwa kuwa haujafanyika ndani ya kipindi cha miaka 17.

Lengo la zoezi hili ni kukusanya takwimu ambazo zitasaidia katika kufikia malengo ya maendeleo ya nchi na kuimarisha maisha ya watu.

Rais pia amepongeza mbinu inayowekwa na tume, ya kufanya sensa sahihi na ya uhakika, hususan utumizi mkubwa wa teknolojia yenye uwezo wa kufanya sensa ya Kimataifa na kuweka misingi endelevu ya sensa zijazo.

Aidha aliiagiza tume hiyo kuendelea na maandalizi ya uendeshaji wa Sensa ya watu na makazi ya mwaka 2023, ili kuendeleza mafanikio ambayo tayari yamerekodiwa na kutoa msingi kwa uongozi unaokuja kuunganisha mafanikio hayo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.