Pata taarifa kuu
USALAMA-JAMII

Kundi la kigaidi la Boko Haram labadili mbinu zake katika eneo la Ziwa Chad

Kundi la Boko Haram limeanzisha mbinu mpya katika ukatili wake, sasa linajihusisha na utekaji nyara ili kupata fidia, jambo ambalo linasababisha watu kuyatoroka makaazi yao. Wakazi wengi wa eneo la Fouli wameanza kuyatoroka makazi yao kutokana na ukatili huo.

Kambi ya Kabelawa, karibu na Diffa, inawa Wanigeria 2,500 waliohamishwa kutoka visiwa vya Ziwa Chad.
Kambi ya Kabelawa, karibu na Diffa, inawa Wanigeria 2,500 waliohamishwa kutoka visiwa vya Ziwa Chad. Pierre Pinto/RFI
Matangazo ya kibiashara

Nchini Chad, utawala, mashirika yasiyo ya kiserikali na waandishi wa habari wanaofanya kazi katika eneo la Ziwa Chad, kusini-magharibi mwa nchi hiyo, wamethibitisha habari hii: kundi la wanajihadi la Boko Haram lilibadilisha mfumo wa harakati zake takriban miezi sita iliyopita. Hakuna tena mashambulizi makubwa kwa miezi kadhaa katika eneo hilo, wanajihadi wa Boko Haram sasa wanafanya kazi usiku na katika makundi madogo ya wapiganaji sita hadi wanane, wakiepuka jeshi la Chad.

"Boko Haram imebadilisha mbinu zake za ukatili wake. Linajihusisha kwa sasa na utekaji nyara dhidi ya wafanyakazi wa serikali na mashirika yasiyo ya kiserikali ili kuwaachilia baada ya kulipwa fidia,” anaeleza mkuu wa wilaya ya Fouli, Adoum Mahamat Mbomi.

Lakini hawa sio walengwa pekee wa wanajihadi wa Boko Haram, anaendelea mkuu wa wilaya ya Fouli. “Wavulana na wasichana wadogo pia. Wakati mwingine wanatoroka kutoka mikononi mwa Boko Haram. Baadhi wanakombolewa baada ya kulipa fidia, na wengine wanachukuliwa kama wapiganaji. Na baadhi ya wasichana hawa wanalazimishwa kuolewa na wanajihadi.

Madhara yake, ukosefu huu wa usalama, pamoja na mafuriko ambayo hivi majuzi yalikumba eneo hili lote la Ziwa Chad, yalisababisha watu wengi kuhamakutoka visiwa vya Ziwa Chad kwenda bara. "Mashiriia yasiyo ya kiserikali yameanza kuingilia kati lakini watu ni wengi", takriban watu 45,000, amebainisha Adoum Mahamat.

Eneo hilo limekuwa la kutisha kiasi kwamba wadau mbalimbali kutoka eneo la Ziwa Chad wamekutana hivi punde katika "Jukwaa dhidi ya ukatili wa Boko Haram" zaidi ya wiki moja iliyopita huko Bol, mji mkuu wa eneo hilo. Wanaiomba serikali kuweka kambi zaidi na doria za kijeshi au kuwapa silaha wawindaji wa ndani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.