Pata taarifa kuu
CHAD-BOKO HARAM-USALAMA

Chad: Wanamgambo 44 wa Boko Haram wapatikana wamekufa katika jela Chad

Wafungwa 44 wa kundi la wapiganaji wa msimamo mkali la Boko Haram waliokamatwa na jeshi la Chad mwanzoni mwa mwezi huu katika mkoa wa Lac wamepatikana wamefariki dunia ktika jela usiku wa Alhamisi kuamkia Ijumaa wiki hii, kulingana na mamlaka.

Wapiganaji wa Boko Haram walikamatwa na jeshi la Chad wakati wa Operesheni iliyoitwa "Hasira ya Bohoma" (picha ya kumbukumbu)
Wapiganaji wa Boko Haram walikamatwa na jeshi la Chad wakati wa Operesheni iliyoitwa "Hasira ya Bohoma" (picha ya kumbukumbu) REUTERS/Stringer
Matangazo ya kibiashara

Wfungwa hao walikabidhiwa mahakama siku ya Jumatano baada ya kukamatwa katika operesheni ya jeshi la Chad dhidi ya shambulio baya lililogharimu maisha ya askari wa chad katika moja ya kambi za jeshi la nchi hiy.

Wafungwa Arobaini na nane kutoka kundi la Boko Haram walizuiliwa katika kituo kimoja nje ya mji mkuu wa Ndjamena na kukabidhiwa mahakama siku ya Jumatano. Lakini Alhamisi asubuhi, 44 kati yao walikutwa wamefariki dunia katika katika chumba waliko kuwa wamezuiliwa, kulingana na mamlaka ya Chad.

Kulingana na uchunguzi wa daktari, wapiganaji hao walikunywa sumu. Ripoti yake ya vipimo, kulingana na taarifa ya mwendesha mashtaka wa Ndjamena, Youssouf Tom, "inaonysha kwamba walitumia vidonge vyenye sumu iliyosababisha kwenye moyo kwa baadhi, huku wengine wakishindwa kupumua" .

Wafungwa kumi na wanne walinusurika , hata hivyo utaratibu wa kisheria unaendelea kuwakabili, kulingana na chanzo cha serikali.

Wote walikamatwa wakati wa operesheni iliyoitwa "Hasira ya Bohoma", iliyotekelezwa na jeshi la Chad kuanzia Machi 31 hadi Aprili 8. Karibu wanajeshi 52 wa Chadi na wapiganaji kadhaa wa Boko Haram waliuawa katika mapigano hayo; baada ay mapigano hayo Rais aw Chad Rais Idriss Déby, alizuru eneo la tukio, na kudai kwamba kundi la kigaidi lilitimuliwa katika ardhi ya Chad.

Operesheni hii ya kijeshi ilikuwa jibu la shambulio la Machi 23, lililotekelezwa na kundi la wapikanaji wa Boko Haram dhidi ya kituo cha jeshi kinacho patikana kwenye kisiwa kidogo cha Bouma, katika eneo la Ziwa Chad, ambapo askari wengi wa Chad waliuawa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.