Pata taarifa kuu
CHAD-BOKO HARAM-USALAMA

Kituo cha jeshi chashambuliwa na Boko Haram katika Jimbo la Ziwa Chad

Ngome za jeshi la Chad zimelengwa na mashambulizi ya kundi la Boko Haram usiku wa Jumapili kuakia Jumatatu Desemba 2 katika Jimbo la Ziwa Chad.

Maeneo yaliyo pembezoni mwa ziwa Chad yameendelea kulengwa na mashambulizi ya Boko Haram, kama kijiji hiki cha Ngouboua, mwezi Aprili mwaka 2015.
Maeneo yaliyo pembezoni mwa ziwa Chad yameendelea kulengwa na mashambulizi ya Boko Haram, kama kijiji hiki cha Ngouboua, mwezi Aprili mwaka 2015. AFP PHOTO / PHILIPPE DESMAZES
Matangazo ya kibiashara

Shambulio hilo ambalo mamlaka nchini Chad inalihusisha kundi la Boko Haram limegharimu misha ya wanajihadi 13, wakati maafisa wawili wa afya na dereva wao waliotekwa nyara na wanamgambo hao wa Kiislamu bado hawajapatikana.

Shambulio hilo lilitokea kati ya Ngouboua na Baga Sola, katika eneo lenye watu ambapo jeshi liliweka kituo chake katika siku za nyuma baada ya daktari, muuguzi na dereva wao kutekwa nyara kwenye barabara hiyo.

Wanajihadi walifanya shambulio la kuvizia kwa kufyatua risasi dhidi ya askari. Wakati huo huo jeshi la Chad lilijibu na kuwatimua washambuliaji, ambao walirudi nyuma na miili 13 ya wapiganaji wenzao. Askari wanne wa Chai waliuawa katika mapigano hayo na wengine watatu kujeruhiwa.

Shambulio hili jipya ambalo limetekelezwa na tawi la kundi la Boko Haram, lenye mafungamano na kundi la Abu Musab al-Barnawi, ambalo linadhibiti eneo la Kaskazini mwa Ziwa Chad, limeamua kubadilisha mkakati wake baada ya kuendesha kwa miezi kadhaa mashambulizi tofauti yakifuatwa na utegaji wa vifaa vya kulipuka.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.