Pata taarifa kuu

Nigeria: Matokeo ya ugavana na wabunge yameanza kutolewa

NAIROBI – Matokeo ya uchaguzi wa ugavana na wabunge uliofanyika mwishoni mwa juma lililopita nchini Nigeria, yameanza kutolewa huku gavana wa jiji la lagos kupitia chama tawala, akifanikiwa kuchaguliwa tena katika uchaguzi uliogubikwa na vurugu pamoja na vitendo vya Rushwa.

Raia nchini Nigeria wamepiga kura kuwachagua wabunge na magavana.
Raia nchini Nigeria wamepiga kura kuwachagua wabunge na magavana. © AFP
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa katiba ya Nigeria , magavana ni miongoni mwa viongozi wenye ushawishi, ambapo husimamia ugavi wa bajeti za majimbo yao ambazo ni kubwa kuliko hata zile za baadhi ya nchi za Afrika.

Aidha uchaguzi wa siku ya Jumamosi, ulihusisha kuchagua magavana 28 na wabunge zaidi ya 900, ambapo ulifanyika ikiwa ni wiki tatu zimepita tangu mgombea wa chama tawala cha APC, Bola Tinubu, atangazwe mshindi.

Uchaguzi wa ugavana kwenye jimbo la Lagos, ulikuwa unatazamwa kwa karibu, hasa baada ya aliyekuwa mgombea urais wa chama cha labour Peter Obi, kushinda idadi ya kura kwenye jimbo hilo dhidi ya Tinubu.

Zoezi hili lilikuwa kipimo kingine kwa chama tawala ikiwa bado kina ushawishi kwa raia au la, licha ya kuwa idadi ya wapiga kura haikuwa kubwa kama ile iliyoshuhudiwa wakati wa uchaguzi wa rais.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.