Pata taarifa kuu

Ethiopia: Blinken aweka masharti ya msaada wa Marekani kwa 'maridhiano' Tigray

Afisa wa ngazi ya juu zaidi wa Marekani kuzuru Ethiopia tangu kuzuka kwa vita huko Tigray mnamo mwezi Novemba 2020, ni Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken ambaye alikutana siku ya Jumatano (Machi 15) na Waziri Mkuu wa Ethiopia, wawakilishi wa waasi wa Tigray, pamoja na mashirika ya kutoa misaada na viongozi wa mashirika yakiraia.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken akiwa na Waziri wa Fedha wa Ethiopia Ahmed Shide kwenye bohari ya Umoja wa Mataifa mjini Addis Ababa, Machi 15, 2023.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken akiwa na Waziri wa Fedha wa Ethiopia Ahmed Shide kwenye bohari ya Umoja wa Mataifa mjini Addis Ababa, Machi 15, 2023. © Tiksa Negeri / Pool via AP
Matangazo ya kibiashara

Na mwandishi wetu wa kanda, Albane Thirouard

Nchi hizo mbili zilikuwa na lengo la kuunda upya uhusiano baada ya miaka miwili ya mzozo, ambao mwisho wake ulitiwa sahihishwa na makubaliano ya amani yaliyotiwa saini mwezi Novemba nchini Afrika Kusini.

Ushiriki wa Marekani nchini Ethiopia utasonga mbele ikiwa nchi hiyo itasonga mbele kwa "maridhiano na uwajibikaji" kwa ukatili uliofanywa wakati wa mzozo huko Tigray, Antony Blinken alitangaza siku ya Jumatano.

Addis Ababa inashinikiza hasa kuondolewa kwa hatua ya kusimamishwa kwake AGOA, sheria inayoruhusu baadhi ya mauzo ya nje kwenda Marekani bila ushuru wa forodha. Nchi hiyo ilisimamiswa mwanzoni mwa mwaka 2022 kwa sababu ya mzozo wa Tigray, jimbo lililokumbwa na uhalifu dhidi ya binadamu, kulingana na Washington.

Lakini leo, wakati mkuu wa diplomasia ya Marekani akisisitiza kwamba makubaliano ya amani yalikuwa yanakwenda "katika mwelekeo sahihi", pia alikumbusha haja ya kuanzisha mchakato wa haki ya mpito "wazi kwa wote na kamili". Ukiukaji wa haki za binadamu huko Tigray lazima pia ukomeshwe kabisa, alisisitiza Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani.

Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed alisema kwenye Twitter kwamba wamekubaliana wakati wa mkutano wao "kuimarisha" uhusiano wa pande mbili kati ya nchi zao mbili. Antony Blinken tayari ametangaza dola milioni 331 za msaada wa kibinadamu kusaidia Waethiopia walioathiriwa na migogoro, ukame na uhaba wa chakula.

Antony Blinken anatarajiwa kukutana tena Alhamisi hii asubuhi na Rais wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika, Moussa Faki Mahamat kabla ya kwenda Niger. Naye Makamu wa Rais wa Marekani Kamala Harris anatarajia kuzuru Ghana, Tanzania na Zambia mwishoni mwa mwezi huu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.