Pata taarifa kuu

DRC: Justicia Asbl yaiomba CENI kuongeza muda wa usajili wa wapiga kura

NAIROBI – Shirika la kiraia la Justicia Asbl linalofanya shughuli zake mjini Lubumbashi nchini DRC, hapo jana limetoa wito kwa tume ya uchaguzi CENI, kuongeza muda wa miezi miwili wa zoezi la kusajili wapiga kura kwenye eneo la Haut-Katanga.

CENI imeongeza muda kuwasajili wapiga kura katika maeneo 15
CENI imeongeza muda kuwasajili wapiga kura katika maeneo 15 © John Wessels - AFP
Matangazo ya kibiashara

Mratibu wa shirika hilo, Tomothee Mbuya, amesema kuna sababu kadhaa za wao kuomba muda kuongezwa ikiwe ari ya raia wanaotaka kushiriki uchaguzi wa mwaka huu.

“Kulikuwa na mambo mengi yasiyoendekea vema na CENI ilitakiwa kurekebisha na kukemea kwa wakati unaofaa, kwa mfano inahusu watu kutoa rushwa ili kuingia katika ofisi ya usajili, uchache wa mashine za kuandika wapigakura na hitilafu za kiufundi, wizi wa vitambulisho vya mpigakura, ndio maana Justicia inamuomba mwenyekiti wa CENI kuongeza muda wa usajili wa wapigakura, na polisi walioko katika ofisi za CENI wabadilishwe kwa wakati ili kuzuia utoaji wa hongo kwenye kuingia katika ofisi za usajili.”amesemaTomothee Mbuya.

Tayari CENI imeongeza muda wa siku kumi na tano zaidi wa zoezi la kuwasajili wapiga kura katika maeneo ya Haut Katanga, Mkowa wa zamani wa Katanga, lakini pia Lomami, mkowani Kasai, Kasai ya kati, Kasai-Oriental, mkowa wa Lualaba, Sankuru, Tanganyika pamoja na nchi Tatu ambazo ni Afrika kusini, Ubelgiji, na Ufaransa.

Raia nchini DRC wanatarajiwa kupiga kura kuwachagua viongozi wao wapya mwakani wengine wakiwa na matumaini kuwa viongozi wao wapya watakaowachaguwa watasaidia kupambana na swala utovu wa usalama ambalo limekuwa changamoto kwa raia wa mashariki ya DRC.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.