Pata taarifa kuu

Waziri wa Mambo ya Nje wa Gabon Michael Moussa Adamo aaga dunia

Waziri wa Mambo ya Nje wa Gabon Michael Moussa Adamo amefariki mjini Libreville siku ya Ijumaa baada ya kupata mshtuko wa moyo wakati wa kikao cha Baraza la Mawaziri, serikali na chanzo kutoka ofisi ya rais vimeliambia shirika la habari la AFP.

Michael Moussa Adamo, Waziri wa Mambo ya Nje wa Gabon, Mei 19, 2022.
Michael Moussa Adamo, Waziri wa Mambo ya Nje wa Gabon, Mei 19, 2022. AFP - ANDREA RENAULT
Matangazo ya kibiashara

Michael Moussa Adamo, mshiika wa karibu wa Rais Ali Bongo Ondimba "amefariki baada ya kupatwa na mshtuko wa moyo" na, "licha ya juhudi za wataalamu", hakuweza kunusurika kifo, kulingana na taarifa fupi ya serikali.

Bw. Moussa Adamo, 62, "alishiriki mwanzoni kwenye kikao cha Baraza la Mawaziri na kuanza kujisikia vibaya," chanzo kilicho karibu na ikulu ya rais kimeliambia shirika la habari la AFP. Amekimbizwa katika hospitali ya kijeshi baada ya "kupoteza fahamu" na kuwekwa katika chumba cha wagonjwa mahututi, alifariki muda mfupi baada ya saa sita mchana, kulingana na chanzo hiki, ambacho kimeomba kutotajwa jina.

"Alikuwa mwanadiplomasia mkubwa sana, mwanasiasa wa kweli. Kwangu mimi, kwanza alikuwa rafiki, mwaminifu na mkweli, ambaye siku zote niliweza kumtegemea. Ni hasara kubwa kwa Gabon", Rais Bongo amesema kwenye ukurasa wake wa Twitter.

Michael Moussa Adamo ambaye alizaliwa Januari 10, 1961 huko Makokou, kaskazini-mashariki, alianza kazi yake mnamo 1981 kama mtangazaji kwenye runinga ya taifa. Akiwa na shahada ya uzamili katika uhusiano wa kimataifa na mawasiliano katika Chuo Kikuu cha Boston, aliteuliwa mwaka wa 2000 kuwa mkurugenzi kwenye ofisi ya Waziri wa Ulinzi, mkuu wa sasa wa nchi.

Alipochaguliwa kuwa rais baada ya kifo cha babake Omar Bongo Ondimba mwaka wa 2009, baada ya kukaa madarakani kwa zaidi ya miaka 41, Bw. Moussa Adamo alikua mshauri wake maalum na msiri wake katika ikulu ya rais kwa miaka kadhaa. Baada ya miaka 10 kama balozi wa Gabon nchini Marekani (2011-2020), aliteuliwa kuwa waziri wa ulinzi mnamo mwezi Julai 2020 kisha wa waziri wa mambo ya nje mnamo mwezi Machi 2022.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.