Pata taarifa kuu

WHO ina wasiwasi kuhusu kucheleweshwa kwa vita dhidi ya homa ya uti wa mgongo ya aina A

Shirika la Afya Duniani, WHO, linasema linatiwa wasiwasi juu ya hatari ya kuibuka tena kwa homa ya uti wa mgongo ukikaribia msimu ambapo maambukizo yanaripotiwa mara kwa mara, ikimaanisha kuanzia mwezi wa Januari.

Meningococcus ni bakteria ambayo inaweza kusababisha ugonjwa wa Uti wa mgongo na aina nyingine za ugonjwa wa meningococcal.
Meningococcus ni bakteria ambayo inaweza kusababisha ugonjwa wa Uti wa mgongo na aina nyingine za ugonjwa wa meningococcal. © Shutterstock / Tatiana Shepeleva
Matangazo ya kibiashara

Wakati ugonjwa wa uti wa mgongo wa kundi A ulikuwa karibu kutokomezwa, kutokana na janga la UVIKO-19 ambalo lilitatiza usafiri na kampeni za chanjo mnamo mwaka 2020 na 2021, watoto milioni 50 katika bara la Afrika hawakuweza kuchanjwa dhidi ya aina hii ya ugonjwa ambao unaweza kusababisha vifo au uharibifu wa ubongo.

Kuzuia, uchunguzi, ufuatiliaji wa milipuko ya kuambukiza... Katika nchi kadhaa, shughuli za afya ya umma katika mapambano dhidi ya homa ya uti wa mgongo zilipunguzwa kwa nusu mwaka wa 2020 ikilinganishwa na mwaka 2019, inabainisha WHO kwa msingi wa ripoti zinazopitishwa na nchi.

Licha ya uboreshaji ulioonekana mnamo mwaka 2021, Shirika la Afya Duniani linatoa wito kwa mataifa yanayohusika kuharakisha hatua zao za kukabiliana na ugonjwa huo hatari.

"Kutokomeza homa ya uti wa mgongo ni mojawapo ya ushindi mkubwa zaidi wa kimatibabu barani Afrika. Hakuna kesi zilizogunduliwa barani humo katika kipindi cha miaka mitano iliyopita. Lakini wakati janga la UVIKO-19 limechelewesha utoaji wa chanjo kwa zaidi ya watoto milioni 50, kuna hatari kubwa kwamba maendeleo haya yatapotea," amesisitiza Dk Matshidiso Moeti, Mkurugenzi wa WHO katika kanda ya Afrika.

Virusi vya ugonjwa wa Uti wa mgongo au bakteria ni kuvimba kwa utando unaozunguka ubongo na uti wa mgongo. Mnamo 1996, ugonjwa wa Uti wa mgongo wa aina ya A iliua watu 250,000, ikiwa ni pamoja na 25,000 katika miezi michache, barani Afrika.

Katika nchi zilizo hatarini, juu ya ukanda wa kijiografia unaoanzia Senegal magharibi hadi Ethiopia mashariki, WHO inatoa wito wa kuunga mkono programu za kuzuia ugonjwa huo na chanjo.

Kulingana na WHO, dola bilioni moja na nusu zitahitajika katika miaka minane ijayo ili kuwa na matumaini ya kushinda homa ya uti wa mgongo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.