Pata taarifa kuu
LIBYA-SIASA

Libya: Mbabe wa kivita Khalifa Haftar atakiwa kuzifidia familia za wahanga wa kivita

Jaji wa mahakama nchini Marekani, amemwagiza mkuu wa jeshi la mashariki mwa Libya, mbabe wa kivita Khalifa Haftar, kuzifidia familia za walalamishi nchini humo wanaodai kuwa aliagiza kuteswa na kuawaua kwa watu wa karibu na familia hizo.

Mbabe wa kivita nchini Libya, Khalifa Haftar
Mbabe wa kivita nchini Libya, Khalifa Haftar REUTERS/Esam Omran Al-Fetori/File Photo
Matangazo ya kibiashara

Jaji wa mahakama moja mjini Virginia, eneo ambalo aliwahi kuishi Haftar kabla ya kurejea nchini Libya, imesema kuwa kiongozi huyo amekosa kushirikiana na mahakama na kwa hivyo ameagizwa kuzilipa familia hizo kutokana na majeraha waliosababishiwa.

Haftar, aliye na uraia pacha wa Marekani na Libya yuko na nafasi ya kukataa rufa dhidi ya uwamuzi huo wa mahakama kubaini kiasi anachoweza kuzilipa familia hizo.

Kesi iliwasilishwa  mahakamani kati ya mwaka wa 2019 na 2020, kwa misingi kuwa Haftar kama kiongozi wa jeshi katika eneo la mashariki mwa Libya, aliamuru kutekelezwa kwa mashambulio ya bomu kwa raia alipotaka kuchukua mji wa Tripoli mwaka wa 2019,ambapo watu wa karibu na walalamishi katika kesi hiyo walifariki.

Mahakama ilikuwa imesitisha kusikizwa kwa kesi hiyo kuelekea uchaguzi  mkuu nchini Libya mwezi Disemba 2021 ambapo iliaanzishwa tena baada uchaguzi huo kucheleweshwa.

Haftar amekuwa akijaribu kutaka mahakama itupilie mbali kesi hivyo kwa misingi kuwa yeye kama kiongozi wa nchi hawezi kushtakiwa.

Libya imekuwa imekumbwa na mzozo kwa uwongozi tangu kuangushwa kwa utawala wa diketeta Moamer Kadhafi'mwaka wa 2011.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.