Pata taarifa kuu

Wanajihadi wawaua watu 23 Kaskazini Mashariki mwa Nigeria

Nchini Nigeria, wanajihadi wamewauwa wanaume 23 katika jimbo la Borno Kaskazini Mashariki mwa nchi hiyo, katika eneo ambalo limeendelea kushuhudia ukosefu wa usalama.

Magaidi wa Boko Haram nchini Nigeria.
Magaidi wa Boko Haram nchini Nigeria. Defencepost
Matangazo ya kibiashara

Wanajihadi kutoka kundi la ISWAP wanaaminiwa kutekeleza mauaji hayo, baada ya wiki hii, kutangaza kuwa lilikuwa limewashiimlia wanaume hao waliokuwa wanasaka vyuma kukuu katika Wilaya ya Dikwa.

Ripoti zinasema, wanaume háo huenda waliuawa siku ya Jumanne, baada ya wanajihadi hao kuharibu mitambo iliyotatiza mawasiliano katika êneo hilo;

Viongozi wa êneo hilo, wanasema wanaume hao walipatikana wakiwa wamekatwa shingo na kuna wengine 24 ambao bado hawajapatikana baada ya kutoweka.

Mwezi uliopita, mauaji mengine ya watu 30 yaliripotiwa katika eneo hilo baada ya kushambuliwa na wanajihadi hao.

Mauaji haya yametokea wakati huu, jeshi la nchi hiyo likisema limeongeza mashambulio dhidi ya wanajihadi na ISWAP na magaidi wa Boko Haram na wamewauwa baadhi ya viongozi wakuu wa makundi hayo mawili.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.