Pata taarifa kuu
AFRIKA KUSINI-USALAMA

Watu 276 wapoteza maisha katika ghasia Afrika Kusini

Serikali ya afrika Kusini imesema kuwa vurugu zilizotokea nchini humo zilisababisha vifo vya watu wasiopungua 276. Idadi hiyo ni zaidi ya ile ya watu 215 iliyotangazwa hapo awali.

Khumbudzo Ntshavheni amesema ghasia na uporaji uliathiri biashara 40,000 katika mkoa wa KwaZulu-Natal.
Khumbudzo Ntshavheni amesema ghasia na uporaji uliathiri biashara 40,000 katika mkoa wa KwaZulu-Natal. © AFP - Marco Longari
Matangazo ya kibiashara

"Tangu machafuko yalipoanza, vifo 234 vinavyohusiana vimerekodiwa huko Kwazulu-Natal (mashariki) hadi sasa," amesema waziri kwenye ofisi ya rais, Khumbudzo Ntshavheni, akiripoti vifo 42 katika jimbo la Gauteng, ambalo linajumuisha miji mikubwa miwili nchini Afrika Kusini, Johannesburg na Pretoria.

Inakadiriwa kuwa athari za kiuchumi katika mkoa wa KwaZulu-Natal pekee ni zaidi ya dola bilioni moja za Kimarekani.

Khumbudzo Ntshavheni amesema ghasia na uporaji uliathiri biashara 40,000 katika mkoa wa KwaZulu-Natal.

Akinukuu data zilizotolewa na chama cha wamiliki mali nchini Afrika Kusini, Khumbudzo Ntshavheni amesema zaidi ya maduka 200 yaliporwa, huku akiongeza kuwa bidhaa za thamani ya zaidi ya dola milioni moja zilipotea mjini Durban pekee.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.