Pata taarifa kuu
LIBYA-MAPIGANO-USALAMA

Wapiganaji kutoka Yemen katika vita vya Libya

Vikisaidiwa na vikosi vya Ankara, kambi ya Fayez el-Sarraj inatafuta kwa nguvu zote kudhibiti mji wa Sirte kabla ya mazungumzo yoyote ya kisiasa au ya kijeshi.

Askari wa serikali ya umoja wa kitaifa, kwenye uwanja wa vita karibu na Misrata, Februari 3, 2020.
Askari wa serikali ya umoja wa kitaifa, kwenye uwanja wa vita karibu na Misrata, Februari 3, 2020. EUTERS/Ayman Al-Sahili
Matangazo ya kibiashara

Uturuki, ambayo tayari imetuma wapiganaji wengi na ndege zisizo na rubani kwenye uwanja wa vita, imetuma pia mamluki wapya kutoka Yemen.

Nchini Libya, vikosi vya Marshal Haftar vimeshindwa kuudhibiti mji wa Tripoli na hivyo vita vya nchini Libya kuingiliwa na mataifa mbalimbali.

Kufikia sasa mataifa kadhaa yameendelea kuhusika katika vita vinavyoendelea nchini Libya. Urusi, Sudan na Chad wanasaidia vikosi vya Marshal Khalifa Haftar (LNA).

Mamluki kutoka Uturuki na maelfu ya raia wanaojiolea kutoka Syria wametumwa na Uturuki kusaidia wanamgambo walio waaminifu kwa serikali ya umoja wa kitaifa (GNA) inayoongozwa na Fayez el-Sarraj. Wakiwa na silaha za kisasa, mamluki hawa kutoka Syria wamebadilisha hali ya mambo kwenye uwanja wa vita.

Mbali na Uturuki sasa Yemen imeingilia kati katika vita vinavyoendelea nchini Libya kwa upande wa vikosi vya serikali inayotambuliwa na Umoja wa Mataifa. Kundi la kwanza la wapiganaji 200 kutoka Yemen waliotumwa na Uturuki waliwasili huko Tripoli mapema wiki hii, ameripoti mwanahabari wetu Houda Ibrahim. Habari hiyo imethibitishwa na vyanzo kadhaa. Makubaliano kati ya Idara ya ujasusi ya Uturuki na chama cha Kiislam cha Yemeni Islah ni haya yafuatavyo: "Mtusaidie nchini Libya na si tutawakusaidia nchini Yemen".

Kulingana na wachunguzi kadhaa, chama hiki cha Kiisilamu kinataka kuunda muungano na Ankara ambao unajiandaa kuingilia kijeshi nchini Yemen.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.