Pata taarifa kuu
UFARANSA-UTURUKI-LIBYA-USALAMA

Ufaransa yaistumu Uturuki kuingiza silaha nchini Libya

Ufaransa imesema imejiondoa katika operesheni ya kiusalama katika jeshi la Umoja wa kujihami wa nchi za Magharibi NATO kutokana na mzozo wake na Uturuki kuhusu hali ya usalama na kisiasa nchini Libya.

Vikosi vya Serikali ya umoja wa kitaifa ya Libya huko Tripoli; Juni 4.
Vikosi vya Serikali ya umoja wa kitaifa ya Libya huko Tripoli; Juni 4. REUTERS/Ayman Al-Sahili
Matangazo ya kibiashara

Vikosi vya Ufaransa vimekuwa vikishiriki katika operesheni katika Bahari ya Guardian na kuishtumu Uturuki kwa kuendelea kukiuka vikwazo vya kuizuia Libya kupata silaha.

Uturuki imesema wazi kuwa inaiunga mkono serikali inayotambuliwa na Umoja wa Mataifa dhidi ya vikosi vya kiongozi wa upinzani Marshal Khalifa Haftar.

Wakati huo huo Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki Mevlut Cavusoglu amesema Alhamisi kuwa Ankara inasubiri msamaha kutoka kwa Ufaransa kwa "tuhuma zake za uwongo" zinazohusiana na tukio lililotokea mwezi uliopita.

Uchunguzi wa NATO haukutilia manani hoja zilizotolewa na Paris, Mevlut Cavusoglu amesema.

"Ufaransa inapaswa kuomba msamaha badala ya kupinga Uturuki na habari za uwongo," Cavusoglu amesema katika mkutano na waandishi wa habari huko Berlin.

Ufaransa inashutumu Uturuki, mshirika wa NATO, kwa kutoheshimu ahadi zake kuhusu Libya. Imeamua kusitisha kwa muda ushiriki wake katika shughuli za uchunguzi wa NATO mashariki mwa bahari ya Mediterranean wakati ikitafuta ufafanuzi kutoka kwa NATO, hasa kwa kuheshimu vikwazo vya silaha kwenda nchini Libya.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.