Pata taarifa kuu
UTURUKI-UFARANSA-USHIRIKIANO

Uturuki kuboresha ushirikiano wa kibiashara na Ufaransa

Rais wa Uturuki Recepp Erdogan atakutana na rais wa Ufaransa Emmanuel Macron, Ijumaa ijayo ziara yenye lengo la kuchochea mahusiano na Umoja wa Ulaya baada ya kipindi cha mwaka 2017.

El presidente de Turquía, Reccep Tayyip Erdogan, durante una ceremonia en Ankara, Turquía, el 21 de diciembre de 2017.
El presidente de Turquía, Reccep Tayyip Erdogan, durante una ceremonia en Ankara, Turquía, el 21 de diciembre de 2017. Kayhan Ozer/Palacio Presidencial
Matangazo ya kibiashara

Taarifa zinasema kuwa Uturuki ikiwa katika harakati za kurejesha uhusiano wake pamoja na umoja wa Ulaya imejaribu kufanya kila mbinu lakini kutokana na msimamo wake kuhusu baadhi ya makubaliano ya ndani uhusiano huo umekuwa si mzuri.

Vyanzo vya kidiplomasia vimesema leo kuwa Mazungumzo kati ya rais Erdogan pamoja na mwenyeji wake ambaye ni rais wa Ufaransa Emmanuel Macron yatafanyika kwenye ikulu ya Champs Elysee, Ijumaa na kwa pamoja watazungumzia mgogoro unaolikumba taifa la Syria, lakini pia uhusiano wa kidiplomasia kati ya Uturuki na Ufaransa kwa namna ya pekee, na namna ya kuboresha uhusiano kati ya Uturuki na umoja wa ulaya.

Rais Macron amesema nchi yake iko tayari kupanga mikakati thabiti ya kuboresha ushirikiano wa kibiashara na Uturuki, katika kufikia malengo ya nchi yake ambayo ni kuinua uchumi wa nchi yake, mwaka huu wa 2018, huku akisema anaamini kuwa Uturuki ni miongoni mwa mataifa ambayoUfaransa itashirikiana kibiashara.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.