Pata taarifa kuu
DRC-KAMERHE-HAKI

Matokeo ya vipimo kuhusu kifo cha jaji katika kesi ya Kamerhe yasubiriwa

Raia nchini DRC wanaendelea kusubiri kujuwa ukweli kuhusu kifo cha jaji Raphaël Yanyi Ovungu, katika muktadha wa kesi dhidi ya aliyekuwa mnadhimu mkuu katika Ofisi ya rais jijini Kinshasa Vital Kamerhe.

Vital Kamerhe, alipigwa picha Novemba 11, 2018 huko Geneva.
Vital Kamerhe, alipigwa picha Novemba 11, 2018 huko Geneva. Fabrice COFFRINI/AFP
Matangazo ya kibiashara

Raphaël Yanyi Ovungu, ni jaji aliyekuwa anasimamia kesi ya Vital Kamerhe na washitakiwa wenzake. Alifariki dunia ghafla usiku wa Jumanne kuamkia Jumatano, Mei 27.

Kwenye mitandao ya kijamii na baadhi ya vyombo vya habari nchini DRC, wanabaini kwamba huenda jaji Raphaël Yanyi Ovungualipewa sumu lakini vyombo vya sheria vya DRC vinasubiri matokeo zaidi ya vipimo.

Kulingana na chanzo kilio karibu na uchunguzi, ni mapema mno kusema kuwa Raphaël Yanyi Ovungu aliuawa kwa sumu na mahakama ndio itaeleza kile kilichotokea kwa jaji Yanyi.

Mwili wa Raphaël Yanyi Ovungu ulifanyiwa vipimo siku ya Ijumaa wiki iliyopita, na timu ya madaktari kutoka DRC imefanya tathmini yao ya kwanza, ambayo ni ripoti ya awali inayotoa wito wa kuendelea na vipimo zaidi, kuchunguza iwapo alipewa sumu kupitia sampuli zilizochukuliwa kutoka kwa mwili wa marehemu.

Vipimo hivyo vitafanyiwa katika maabara nchini DRC, chanzo kilio karibu na uchunguzi kimebaini.

Lakini ili kupata matokeo, itachukuwa muda zaidi... labda hata zaidi ya siku 15.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.