Mahakama ya Cote d'Ivoire yamhukumu kifungo cha miaka 20 Charles Ble Goude
Kiongozi wa zamani wa kisiasa nchini Cote d'Ivoire Charles Ble Goude amesema amehukumiwa jela miaka 20 kwa makosa ya mauaji, ubakaji na mateso, hukumu aliyopewa akiwa nje ya nchi hiyo.
Imechapishwa:
Kabla ya hukumu hii Ble Goude ambaye alikuwa mshirika wa karibu rais wa zamani Laurent Gbagbo na kiongozi wa vijana katika chama tawala wakati huo nchini Cote d'Ivoire, alikuwa ameondolewa mashtaka katika Mahakama ya Kimataifa ya ICC.
Licha ya uamuzi huo wa ICC, serikali ya Cote d'Ivoire ilimfungulia mashtaka mapya dhidi yake, kwa madai ya kutekeleza tuhuma hizo wakati wa mzozo wa kisiasa kati ya mwaka 2010-2011.
Mwanasiasa huyo licha ya kuondolewa mashtaka, bado yupo nchini Uholanzi wakati huu ofisi ya kiongozi wa mashtaka katika Mahakama ya ICC ikitarajiwa kukataa rufaa.
Machafuko ya kisiasa nchini Cote d'Ivoire yalisababisha vifo vya zaidi ya watu 3,000.