Pata taarifa kuu
ICC-GBAGBO-HAKI

ICC: Laurent Gbagbo na Charles Blé Goudé wasubiri uamuzi wa mwendesha mashtaka

Mwendesha mashtaka wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu, ICC, Fatou Bensouda, anasubiriwa hadi usiku wa manane leo Jumatatu, Septemba 16 kusema ikiwa atakata rufaa au la kwa kuachiliwa kwa dhamana Laurent Gbagbo na Charles Blé Goudé, ambao waliachiliwa Januari 15.

Charles Blé Goudé (kushoto) na Laurent Gbagbo (kulia)
Charles Blé Goudé (kushoto) na Laurent Gbagbo (kulia) © Photos : AFP/Reuters/Montage RFI
Matangazo ya kibiashara

Rais wa zamani wa Cote d'Ivoire, ambaye bado yuko Brussels chini ya usimamizi wa mahakama, hadi sasa hajaruhusiwa na ICC kuondoka mji mkuu wa Ubelgiji.

Kufutana na uchaguzi wa urais uliopangwa kufanyika mnamo mwezi Oktoba 2020, uamuzi wa Fatou Bensouda unasubiriwa kwa hamu na gamu nchini Côte d'Ivoire kwa sababu ikiwa mwendesha mashtaka ataamua kukata rufaa, Laurent Gbagbo hataweza kuondoka Brussels.

Licha ya kuachiliwa huru, Laurent Gbagbo amewekwa chini ya usimamizi wa mahakama na hawezi kuondoka nje ya mji mkuu wa Ubelgiji bila idhini ya mahakama. Vivyo hivyo kwa Charles Blé Goudé ambaye bado yuko mjini Hague.

Wawili hao wanapaswa kufutiwa uamuzi wa kuwekewa masharti kwa kuachiliwa kwao.

Ikiwa mwendesha mashtaka atakata rufaa, sheria za mahakama ya ICC hazitoi tarehe yoyote ya mwisho kwa uamuzi wa mwisho lakini utaratibu utachukua miezi kadhaa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.