Pata taarifa kuu
UFARANSA-KENYA-USHIRIKIANO

Emmanuel Macron azuru Nairobi: Ziara ya kwanza ya rais wa Ufaransa nchini Kenya

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron anaendelea na ziara yake Afrika Mashariki. Baada ya ziara yake nchini Ethiopia, ambapo rais wa Ufaransa ameonyesha ushirikiano wake kwa mshirika mpya, Waziri Mkuu Abiy Ahmed, leo Jumatano amewasili nchini Kenya.

Rais Macron amewasili jijini Nairobi Jumatano hii, Machi 13, mchana.  Kenya ni nchi ya tatu ambayo rais Macron anazuru, bada ya Djibouti na Ethiopia.
Rais Macron amewasili jijini Nairobi Jumatano hii, Machi 13, mchana. Kenya ni nchi ya tatu ambayo rais Macron anazuru, bada ya Djibouti na Ethiopia. © REUTERS/Thomas Mukoya
Matangazo ya kibiashara

Rais wa Ufaransa amewasili mchana nchini Kenya. Ziara ya kipekee ya saa thelathini na sita.

Hii ni mara ya kwanza rais wa Ufaransa kuzuru Kenya kwa ziara ya kiserikali tangu kupata uhuru wake miaka 56 iliyopita.

Emmanuel Macron, kwa mara nyingine ameonyesha nia yake ya kurejesha sera ya Ufaransa kwa Afrika kuelekea nchi nyingi zaidi, hususan nchi zinazozungumza Kiingereza.

Kuzungumza na wale wanaohusika leo ni kuelekea kwa nchi hii ya watu milioni 50, yenye ukuaji wa watu zaidi ya 5% kwa mwaka.

Rais Macron anataka kuonyesha ujuzi wa makampuni ya Ufaransa. Katika ziara hiyo ameongozana na Wakuu wa makampuni ya GE-Alstom, EDF, Egis na Danone. Mikataba yenye thamani ya euro bilioni tatu itasainiwa, kwa mujibu wa chanzo cha serikali ya Ufaransa.

Rais Macron anatarajia kukutana kwa mazungumzo na rais wa Kenya Uhuru Kenyatta, kisha kesho Alhamisi, Machi 14 anatarajia kushiriki mkutano wa One Planet Summit kabal ya kukutana kwa mazungumzo na wanafunzi katika Chuo Kikuu cha Nairobi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.