Pata taarifa kuu
CAMEROON-EU-SIASA-USALAMA

Umoja wa Ulaya wamtaka Paul Biya kurejesha umoja na mshikamano Cameroon

Umoja wa Ulaya juma hili umemtaka rais mteule wa Cameroon, Paul Biya kuiunganisha nchi yake na kutatua changamoto zinazoripotiwa baada ya kumalizika kwa uchaguzi mkuu wa October 7.

Polisi akitoa ulinzi Bamenda, katikati mwa Jimbo lonalozungumza Kiingereza.
Polisi akitoa ulinzi Bamenda, katikati mwa Jimbo lonalozungumza Kiingereza. Reinnier KAZE/AFP
Matangazo ya kibiashara

Haya yanajiri wakati huu vuguvugu linalodai kujitenga kwa eneo linalozungumza Kingereza wakitupilia mbali takwimu za Serikali iliyodai kuwa watu 10 walipoteza maisha katika makabiliano ya hivi karibuni.

Mashahidi wanasema kuwa makabiliano kati ya vikosi vya usalama na wanaharakati wanaotaka eneo lao kuwa taifa huru siku ya Alhamisi katika mji wa Bambui yalisababisha kifo cha mhadhiri mmoja wa Chuo Kikuu cha Bambili.

"Profesa Mbufong alipigwa risasi wakati alipokuwa akielekea kazini. alifariki dunia muda mfupi baada ya kufikishwa hospitalini huko Bamenda, kwa mujibu wa VOA Afrique ikinukuu chanzo ambacho hakikutaja jina.

Watu kadhaa wameuawa katika makabiliano kati ya polisi na wanaharakati wanaotaka eneo lao kuwa taifa huru, tangu kuanza kwa ghasia hizo nchini Cameroon, hasa katika maeneo yanayozungumza Kiingereza.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.