Pata taarifa kuu
DRC-USALAMA

Mashirika ya kiraia yawataka wakaazi wa Beni kuendelea na maombolezo

Muungano wa mashirika ya kiraia mjini Beni mkoani Kivu Kaskazini yametowa wito kwa wananchi wa eneo hilo kuongeza siku za mambolezo hadi Ijumaa wiki hii.

Askari wa Monusco wakishirikiana na askari wa DRC FARDC wakati wa operesheni katika eneo la Beni, Oktoba 2017.
Askari wa Monusco wakishirikiana na askari wa DRC FARDC wakati wa operesheni katika eneo la Beni, Oktoba 2017. MONUSCO
Matangazo ya kibiashara

Mashirika hayo pia yameomba viongozi wa kiraia na wa kijeshi katika eneo hilo kujiuzulu baada ya kushindwa kuzuia shambulizi dhidi ya raia mwishoni mwa juma lililopita ambalo lilitekelezwa na waasi wa ADF.

Watu 21 walipoteza maisha, wakiwemo raia 17 na wanajeshi 4.

Ripoti ya awali iliyotolewa Jumapili jioni ilibaini kwamba watu 18 sawa na raia 14 na askari wanne waliuawa.

Hali ya utulivu ilishuhudiwa siku ya Jumatatu ambapo hapakuwa na shughuli yoyote, na huenda ikaendelea kushuhudiwa hadi Ijumaa Septemba 28.

Hata hivyo swali limeibuka kuhusu uwezo wa wapiganaji wa ADF waliofaulu kuingia mjini kati, licha ya vizuizi vya jeshi la serikali na vikosi vya Umoja wa Mataifa, Monusco, na kutekeleza mauaji kisha kuondoka bila usumbufu wowote.

Hayo yanajiri wakati ambapo hatma ya wakimbizi wa ndani wa kambi ya Tanganyika imeendelea kuwa matatani baada ya serikali kuvunja kambi yao na kuwataka kurejea makwao, huku wakimbizi hao wakiendelea kuilalamikia serikali kwa kutumia nguvu wakati ambapo baadhi ya maeneo hali ya usalama bado ni tete.

Mashirika ya kiraia yanailaumu serikali kwa kutumia nguvu dhidi ya wakimbizi hao, huku Bernard Biondo Waziri wa Mshikamano na Haki za Kibinadamu anasema hawajamfukuza mtu bali vurugu zilizozuka ni pale jeshi lilipokwedna kuwakamata wahalifu waliojificha kambini na silaha.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.