Pata taarifa kuu
MADAGASCAR-USALAMA

Maandamano mapya dhidi ya utawala yaibuka Madagascar

Wafuasi 2,000 wa upinzani nchini Madagascar wameingia mitaani Jumatano wiki hii kama mwanzo wa maandamano makubwa yaliyoitishwa na upinzani dhidi ya serikali ya nchi hiyo.

Waandamanaji katika mitaa ya Antananarivo, Madagascar, Aprili 23, 2018.
Waandamanaji katika mitaa ya Antananarivo, Madagascar, Aprili 23, 2018. AFP
Matangazo ya kibiashara

Wafuasi wa upinzani wamekua wakiandamana kuelekea makao makuu ya Mahakama ya Katiba mjini Antananarivo, kuwasilisha ombi la kujiuzulu kwa Rais Hery Rajaonarimampianina.

Waandamanaji walikusanyika kwenye eneo la Mei 13, huku wakipiga kelelea na kusema "Rajao jiuzulu mara moja!", mwandishi wa habari washirika la habari la AFP amebaini.

Ikiwa imesalia miezi saba kabla ya duru ya kwanza ya uchaguzi mkuu, upinzani umekua ukiingia mitaani katika mji mkuu wa nchi hiyo kwa muda wa siku tano mfululizo wakipinga sheria mpya za uchaguzi, ambazo wanadai kwamba zimegemea upande wa serikali pekee.

Jumanne wiki hii, wabunge wa upinzani waliomba rais Rajaonarimampiania kujiuzulu, wakimshtumu kutaka kuwazuia wapinzani wake.

Siku ya Jumamosi, maandamano yaliyopigwa marufuku na serikali, yalisababisha makabiliano makubwa kati ya waandamanaji, jeshi na polisi.

Kwa mujibu wa ripoti kutoka chanzo cha hospitali, makabiliano hayo yalisababisha vifo vya watu wawili na wengine 16 kujeruhiwa upande wa waandamanaji, ambao wanashtumu vikosi vya usalama kufyatua risasi za moto.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.