Pata taarifa kuu
TOGO-MAANDAMANO-USALAMA

Togo yakabiliwa na maandamano ya upinzani

Upinzani nchini Togo umeitisha maandamano tena leo jijini Lome baada ya kushuhudiwa kwa maandamano makubwa hapo jana kuomba mabadiliko na utekelezwaji wa vifungo vya sheria ya katiba ya nchi hiyo.

Maandamano ya upinzani Septemba 6, 2017 nchini Togo.
Maandamano ya upinzani Septemba 6, 2017 nchini Togo. PIUS UTOMI EKPEI / AFP
Matangazo ya kibiashara

Licha ya serikali kuwasilisha muswada wa sheria unaogiza kuweka kikomo kwa uongozi na mfumo wa uchaguzi wa duru mbili, upinzani unaona kwamba ni maneno matupu ambayo imekuwa vigimu kutekeleza.

Kiongozi mkuu wa Upinzani Tikpi Atchadam amesema wanachodai ni kuona mfumo wa uchaguzi unabadilishwa na kuwa wa duru mbili pamoja na uwepo wa kikomo cha uongozi kwa mihula miwili ya miaka mitano kila mmoja.

Upinzani nchini humo unamtuhumu rais Faure Nyasimbe kuongoza nchi kidikteta. Hata hivyo maandamano hayo yalioshuhudiwa katika maeneo mengi ya nchi hiyo yamefanyika katika hali tulivu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.