Pata taarifa kuu
TOGO-SIASA

Mwanasiasa wa upinzani nchini Togo ahukumiwa miaka 5 jela

Mwanasiasa wa upinzani nchini Togo, Alberto Olympio, amehukumiwa kifungo cha miaka mitano jela na mahakam ya nchi hiyo, kwa ubadhirifu wa Faranga (CFA) bilioni sita. Uamuzi wa kesi ya kiongozi wa chama cha kisiasa nchini Togo ulitolewa Jumatano Septemba 21 na Mahakama ya Jinai ya mjini Lome.

Alberto Olympio mwanasiasa akiwa pia mfanyabiashara nchini Togo.
Alberto Olympio mwanasiasa akiwa pia mfanyabiashara nchini Togo. Google
Matangazo ya kibiashara

Kesi hiyo inahusisha madai ya kibiashara dhidi ya kundi maalumu katika mambo ya mawasiliano ya simu, kulingana na viongozi wa chama chake.

Alberto Olympio hakuwepo wakati uamuzi huo ulitolewa.

Ametakiwa kulipa faranga (CAF) bilioni 5.9 kwa washirika wake wa zamani na kulipa faranga (CFA) milioni 885 kwa uharibifu na fidia.

"Bw Olympio amekumbusha kwamba hatambui kosa lolote ambalo mahakama ya Togo imemuhukumu," Mkurugenzi wake, Nathaniel Olympio, ameliambia shirika la habari la AFP.

Alberto Olympio, mfanyabiashara, alitangaza kuwania katika uchaguzi wa urais wa Aprili 2015 nchini Togo, lakini alijiondoa katika kinyang'anyiro hiki, akibaini kwamba daftari la wapiga kura lilikua limejaa.

Alberto Olympio ni mpwa wa Gilchrist Olympio, mwanasiasa wa upinzani aliyejiunga na utawala miaka michache iliyopita.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.