Pata taarifa kuu
MAREKANI-SIASA

Mwanamke wa kwanza mwenye asili ya Somalia achaguliwa mbunge nchini Marekani

Mbunge wa kwanza mwenye asili ya Somalia, amechaguliwa kutoka katika jimbo la Minnesota nchini Marekani, eneo ambalo kuna idadi kubwa la raia wa Marekani wenye asili ya Somalia.

Ilhan Omar mwanamke wa kwanza mwenye asili ya Somalia kuchaguliwa mbunge nchini Marekani
Ilhan Omar mwanamke wa kwanza mwenye asili ya Somalia kuchaguliwa mbunge nchini Marekani stmedia.startribune.com
Matangazo ya kibiashara

Ilhan Omar mwenye umri wa miaka 33 ameingia katika historia ya nchi hiyo, na kuwa mwanamke wa kwanza kushikilia nafasi hiyo kutoka katika jamii ndogo ya Wasomali.

Ilhan ambaye aliingia Marekani na miaka 8 kama wakimbizi akiwa na familia yake, amekuwa akifahamika sana kwa kutetea haki za binadamu lakini pia wanawake na anafahamika sana kwa mtindo wake wa kuvaa hijab.

Hadi kuchaguliwa kwake, amekuwa akishirikiana na chama cha Democratic na kuingia kwake bungeni kumeleta matumaini kwa jamii ya Somalia ambao wamekuwa wakihisi kutopewa kipau mbele nchini humo.

Wakati wa kipindi cha kampeni, Donald Trump ambaye ameshinda Uchaguzi wa urais aliwashtumu watu wenye asili ya Somalia kwa kuchangia ukosefu wa usalama katika jimbo hilo na kujiunga na makundi ya Islamic State.

Takwimu za mwaka 2010, zinaonesha kuwa jamii ya Wasomalia ina watu 25,000 nchini humo na hasa katika jimbo hilo la Minnesota.

Kuhusu ushindi wa Trump, mbunge huyo mpya amesema haifahamiki ni kitu gani kitafanyika na kuongeza kuwa huu ndio wakati wa jamii hiyo kuanza kujipanga upya.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.