Pata taarifa kuu
ICC-COTE D"IVOIRE-SHERIA-HAKI

ICC: ushahidi tosha kwa kumuhukumu Blé Goudé

Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ICC imetangaza uamuzi wake wa kumfungulia mashataka Waziri wa zamani wa vijana, Charles Blé Goudé, anayetuhumiwa kwa uhalifu dhidi ya ubinadamu wakati wa ghasia za baada ya uchaguzi nchini Côte d’Ivoire.

Charles Blé Goudé, mbele ya Mahakama ya kimataifa ya Jinai ICC, Oktoba 2 mwaka 2014.
Charles Blé Goudé, mbele ya Mahakama ya kimataifa ya Jinai ICC, Oktoba 2 mwaka 2014. ICC-CPI
Matangazo ya kibiashara

Mahakama hiyo imethibitisha kwamba ina ushahidi tosha kuwa Blé Goudé alihusika katika machafuko yaliyotokea Côte d’Ivoire, baada ya uchaguzi.

Uamuzi muhimu ulichukuliwa Alhamisi Desemba 11. Kitengo cha mwanzo cha Mahakama hiyo kimethibitisha kuwa Blé Goudé anakabiliwa na makosa 4 ya uhalifu, ikiwa ni pamoja na mauaji, ubakaji, ukiukwaji wa haki za binadamu na mateso. Kiongozi huyo wa zamani wa vijana wa chama cha FPI cha Laurent Gbagbo, bado ana nafasi ya kukata rufaa.

Wakati huo huo Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ICC imeitaka serikali ya Côte d’Ivoire kumfikisha kwenye Mahakama hiyo Simone Gbagbo, mke wa rais wa zamani Laurent Gbagbo ambaye yuko kizuizini kwa uhalifu dhidi ya ubinadamu.

Mwaka 2012, Mahakama hiyo ilitoa hati ya kukamamtwa dhidi ya Simone Gbagbo kwa tuhuma za mauaji, ubakaji na vitendo vingine vya kinyama ikiwa ni pamoja na mateso wakati wa machafuko yaliyotokea baada ya uchaguzi kati ya Desemba mwaka 2010 na Aprili mwaka 2011.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.