Pata taarifa kuu
KENYA-UGAIDI-USALAMA

Joseph Ole Lenku aachishwa kazi

Rais wa Kenya uhuru Kenyatta amempendekeza meja jenerali mstaafu Joseph Nkaissery kuchukua nafasi ya waziri wa mambo ya ndani, baada ya Joseph Ole Lenku kuachishwa kazi kwenye wadhifa huo.

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta amempendekeza meja jenerali mstaafu Joseph Nkaissery kuchukua ya waziri wa mambo ya ndani.
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta amempendekeza meja jenerali mstaafu Joseph Nkaissery kuchukua ya waziri wa mambo ya ndani. REUTERS/Stringer
Matangazo ya kibiashara

Hayo yanajiri baada ya inspekta jenerali wa polisi nchini Kenya David Kimaiyo kuamua kustaafu mapema kutokana na visa vya mdororo wa usalama ambavyo vinaendelea kushuhudiwa nchini humo.

Rais wa Kenya amechukua uamzi huo, baada ya watu 36 kuuawa usiku wa Jumatatu Desemba 1 kuamkia Jumanne Desemba 2 katika eneo la Mandera kwenye mpaka na Somalia.

Shambulio hilo limetokea karibu na eneo la Arabyia ambapo abiria 28 waliokua ndani basi waliuawa siku kumi ziliyopita.

Shambulio la sasa limeendeshwa na watu waliojifananisha na wachimba migodi katika migodi ya makampuni ya ujenzi. Watu hao walikua wakilala katika hema zao kwenye eneo ambapo hakuna umeme.

Kawaida watu wanaoendesha shughuli hiyo ya kuchimba migodi ni kutoka jamii ya Kikuyu, Kamba,Luo au Luhya, na wengi wao ni kutoka jamii ya Wakristo. Ushahidi mpya unaonesha kuwa washambuliaji hao wamekua wanajua eneo hilo kama limekua likitumiwa na wafanyakazi wanaochimba mawe kutoka jamii hizo.

Taarifa kutoka Ikulu ya Kenya imesema kuwa manusura wacahche wamezungumzia kuwa wamewaona magaidi ishirini miongoni mwa watu waliowashambulia.

Inaonekana kwamba, kama ilivyo kuwa katika mashambulizi ya awali, huenda washambuliaji waliwatenganisha Waislam na Wakristo. Wengi wa waliouawa walipigwa risasi kichwani. Kwa mujibu wa kiongozi wa Shirika la msalaba mwekundu, Abbas koromeo, ambaye ametembelea eneo la tukio, miili ya watu waliouawa imehifadhiwa katika kambi ya jeshi ya Mandera ili iweze kusafirishwa kwa ndege.

Mauaji haya yanatokea wakati hivi karibuni, serikali ya Kenya imekua ikikosolewa kushindwa kukabiliana na tishio la kigaidi. Kwa muda wa miezi kadhaa, wito umekua ukitolea wa kutaka Waziri wa mambo ya ndani na mkuu wa polisi wajiuzulu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.