Pata taarifa kuu
TANZANIA-KATIBA

Rais Jakaya Kikwete awaonya wabunge wa bunge la katiba kuhusu mgawanyiko

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alihutubia bunge maalumu la Katiba na kutaka wajumbe wa bunge hilo kuhakikisha kuwa katiba inayopatikana itakuwa ni katiba yenye Kuheshimu haki za binadamu, kudumisha upendo,katiba inayo tekelezeka, na wananchi kunufaika na maendeleo yatakayo patikana kutokana na katiba hiyo.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete rfikiswahili
Matangazo ya kibiashara

Aidha amewataka wajumbe hao kusoma na kuelewa kilichoandikwa na kufanya uamuzi mzuri wa mawazo yao binafsi pasipo kushauriwa na wenzao ama makundi .

Rais Kikwete amesema kuwa wajumbe hao wana wanawajibu wa kuchambua kwa kina rasimu hiyo ya pili ya katiba kifungu kwa kifungu, ibara kwa ibara, sentensi kwa sentensi, neno kwa neno, na kuboresha pale wanapoona panastahili maboresho na ikiwa kuna jambo ambalo halifai wanao wajibu wa kuliondoa ili kupata katiba itakayo dumu kwa muda mrefu.

Hii ni mara ya tatu kwa Tanzania kufanya mchakato wa kuwa na katiba mpya ambapo mwaka 1965 iliandaliwa katiba ya muda na mwaka 1977 katiba ya kudumu ilitengenezwa ambayo ndiyo inatumika hadi sasa.

Mchakato wa sasa wa katiba mpya ya Tanzania kwa mara ya kwanza umewashirikisha wananchi ambao ndio watakuwa waamuzi wa mwisho kuhusu katiba hiyo kwa kupiga kura ya maoni.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.