Pata taarifa kuu
KENYA-SIASA

Raia wa Kenya wasema kusumbuka kwa kupata kadi ya kupiga kura

Kuelekea uchaguzi Mkuu mwaka ujao nchini Kenya, raia wa nchi hiyo ambao hajajiandikisha wamekuwa wakihangaika kupata vitambulisho vya taifa ili kupata kadi ya kupiga kura.

Askari wa kikosi cha GSU wakipiga doria katika mtaa mmoja mjini MombasaJuni 10, 2014.
Askari wa kikosi cha GSU wakipiga doria katika mtaa mmoja mjini MombasaJuni 10, 2014. REUTERS/Joseph Okanga
Matangazo ya kibiashara

Wakaazi wa Pwani wanasema kupata kitambulisho imekuwa kazi ngumu kwao.

Kwa mujibu wa sheria za nchi ya Kenya, kijana aliyefikisha umri wa miaka 18 anatakikana kupata kitambulisho cha taifa.

Vijana waliofikisha umri huo, wametoa kero zao wakilalamika kuwa wanahangaishwa wakati wanapotafuta stakabadhi hiyo muhimu.

Rais wa Bunge la vijana katika serikali ya kaunti ya Mombasa, Ali Sudi Ali aliingilia kati kuwasaidia vijana wanaokabiliwa na changamoto za kupata vitambulisho.

Gavana wa serikali ya kaunti ya Mombasa Hassan Ali Joho, pia ametoa mwito kwa viongozi kuwasaidia vijana kupata vitambulisho. 

Hata hivyo Rais wa Bunge la vijana katika serikali ya kaunti ya Mombasa, Ali Sudi Ali pia amewalaumiwa vijana hao kwa kutowajibika vilivyo.

Kwa upande wao wananchi walitoa hisia zao kwa kushtumu kamati za kukagua nyaraka za wale wanaotaka vitambulisho.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.