Pata taarifa kuu
KENYA

UTAFITI; Asilimia kubwa ya Wakenya wanakunywa pombe kupindukia

Utafiti uliofanywa nchini Kenya unaonesha kuwa, watu wenye kipato cha juu ndio hunywa pombe kwa kiasi kikubwa na kila panapokuwa na wanaume saba kwenye Bar, kuna mwanamke pia.

Watu wakitembea katikati mwa jiji la Nairobi.
Watu wakitembea katikati mwa jiji la Nairobi. DR
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa utafiti huu uliofanywa na wizara ya afya nchini Kenya, umeongeza kuwa raia milioni 6 wa Kenya ni wanywaji waliopindukia wa vilevi.

Utafiti huu umeonesha kuwa, miongoni mwao watu ambao huwa wanafurahia kunywa vilevi, asilimia 24 ni watu matajiri na asilimia 18 ni watu masikini au wenye kipato cha chini, huku asilimia 50 kati yao, sio masikini wala matajiri.

Matokeo ya utafiti huu yametokana na mahojianok yaliyofanywa ana kwa ana na wahojiwa elfu 45 wenye umri wa kati ya miaka 18 na 69.

Licha ya kuwa utafiti huu ulilenga kutoa mwanga kuhusu uhusiano kati ya watumiaji wa vilevi na magonjwa ya kuambukiza, umeonesha pia asilimia 13 ya Wakenya wameathiriwa na ulevi na hawawezi kuacha kunywa.

Hata hivyo asilimia ya watu wanaotumia vilevi hatari huenda ikawa ni kubwa zaidi hata kufikia asilimia 36 na idadi kubwa ya watu hawa wanapatikana kwenye maeneo ya vijijini ambako pombe hizi kupatikana kwa wingi.

Utafiti huu umekuwa ni wa kwanza kufanyika nchini Kenya kuhusu magonjwa yasiyoambukiza.

Daktari Gladwell Gathecha kutoka kitengo cha magonjwa yasiyoambukiza kwenye wizara ya afya, amesema kuwa, lengo lilikuwa ni kubainik hatari zinazowakabili watumiaji wa vilevi na mazingira yanayoweza kuwasababisha kupata maambukizik ya magonjwa, ili waweze kuandaa mpango wa kuzuia.

Utafiti umeonesha kuwa kwa sehemu kubwa watumiajik wa vilevi wamekuwa wakipata maambukizik yanayoweza kuepukika kutokana na kutotumia mboga za majani na matunda.

Ni asilimia 6 tu ya Wakenya ndio wenye uwezo wa kupata vitamini kutoka kwenye mlo kamili, huku asilimia 94 hawana uwezo huo.

Utafiti huo umeongeza kuwa asilimia 84 ya Wakenya hupendelea kuongeza chumvi na Sukari nyingi wakati wa uandaaji wa chakula majumbanik mwao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.