Pata taarifa kuu
KENYA

Tume ya huduma za mahakama, JSC yapendekeza David Maranga kuteuliwa kuwa jaji mkuu Kenya

Tume ya huduma ya Mahakama nchini Kenya JSC, imemteua David Maraga ambaye anahudumu kama Jaji wa Mahakama ya rufaa mjini Kisumu Magharibi mwa nchi hiyo kuwa Jaji Mkuu na rais wa Mahakama ya Juu.

David Maraga, ambaye ameteuliwa na tume ya huduma za mahakama kuchukua nafasi ya jaji Mutunga, sasa anasubiri kuidhinishwa na bunge na kupitishwa na rais Kenyatta.
David Maraga, ambaye ameteuliwa na tume ya huduma za mahakama kuchukua nafasi ya jaji Mutunga, sasa anasubiri kuidhinishwa na bunge na kupitishwa na rais Kenyatta. www.judiciary.go.ke
Matangazo ya kibiashara

Maraga mwenye umri wa miaka 65, atachukua nafasi ya Willy Mutunga aliyestaafu mwezi Juni, mwaka mmoja kabla ya muda wake kufika mwisho.

Hata hivyo, kabla ya kuanza kazi atathibitishwa na Bunge na kuteuliwa rasmi na rais Uhuru Kenyatta.

Jaji huyo aliwashinda wagombea wengine 13 wakiwemo Majaji wa Mahakama ya Juu, Smokin Wanjala, Jakcton Ojwang, msomi Profesa Makau Mutua na wengine waliokuwa wanapewa nafasi kubwa kumrithi Mutunga.

Kabla ya kuteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama kuu na Mahakama ya Rufaa, Jaji Maraga alikuwa wakili kwa zaidi ya miaka 20.

Kuwepo kwa Jaji Mkuu nchini Kenya, ni muhimu sana nchini humo kuelekea Uchaguzi Mkuu mwaka ujao utakaofanyika mwezi Agosti.

Mwaka 2013, muungano wa upinzani CORD, ulikwenda Mahakamani kupinga ushindi wa Uhuru Kenyatta lakini Majaji wa Mahakama hiyo wakaamua kwa pamoja kuwa mshindi halali alikuwa ni Kenyatta.

Wakenya wameanza kupata imani na idara ya Mahakama baada ya kupata katiba mpya mwaka 2010, na kuundwa kwa Mahakama ya juu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.