Pata taarifa kuu
TOGO-AU-ECOWAS-UCHAGUZI-SIASA-USALAMA

Umoja wa Afrika na ECOWAS wakaribisha zoezi la upigaji kura Togo

Usiku wa Jumapili kuamkia Jumatatu wiki hii, Tume huru ya kitaifa ya uchaguzi nchini Togo, CENI, ilimtangaza Faure Gnassingbé mshindi katika uchaguzi wa urais uliofanyika Jumamosi Februari 22, 2020 nchini humo.

Maafisa wa tume huru ya kitaifa ya uchaguzi wakati wa zoezi la kuhesabu kura katika kituo cha kupigia kura huko Lomé, Februari 22, 2020 (picha ya kumbukumbu).
Maafisa wa tume huru ya kitaifa ya uchaguzi wakati wa zoezi la kuhesabu kura katika kituo cha kupigia kura huko Lomé, Februari 22, 2020 (picha ya kumbukumbu). YANICK FOLLY / AFP
Matangazo ya kibiashara

Ujumbe wa Umoja wa Afrika na ule wa Jumuiya ya kiuchumi ya nchi za Magharibi, ECOWAS, wamekaribisha jinsi uchaguzi huo ulivyofanyika katika mazingira mazuri.

Jumatatu alasiri ujumbe wa ECOWAS ulisema kwamba mchakato wa uchaguzi uliopelekea kufanyika kwa uchaguzi wa Februari 22 "ullifanyika katika mazingira mazyri, na hapakuepo na matukio mabaya makubwa". Mchakato ambao "ulifanyika kwa amani na kwa mujibu wa sheria za uchaguzi," alisema Francis Béhanzin, Kamishna wa ECOWAS anayehusika na Masuala ya Siasa, ambaye alijumuika na ujumbe huo ulioongozwa na rais wa zamani wa Sierra Ernest Bai Koroma.

Taasisi hii iliwatuma waangalizi 79 katika mikoa mitano ya nchi ili kuangalia uchaguzi ambao ulifanyika katika vituo zaidi ya 9,300 vya kupigia kura.

Kwa upande wake, ujumbe wa Umoja wa Afrika umepongeza "raia, serikali, wanasiasa na wadau wote katika mchakato huo. Ujumbe huo pia unasema haukushuhudia matukio mabaya makubwa.

Waziri wa Usalama wa Togo Yark Damehane, amekaribisha ripoti hiyo Jumuiya ya kiuchumi ya nchi za Magharibi mwa Afrika. "ECOWAS imeelezea tu kile ilichoona, ni hatua nzuri kwa nchi yetu."

Hata hivyo upinzani umefutilia mbali ripoti hizo na kubaini kwamba uchaguzi uligubikwa na udanganyifu mkubwa wa kura.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.