Pata taarifa kuu

Familia ya Navalny yaishutumu Urusi kwa kuficha mwili wake ili 'kuwalinda' 'wauaji'

Wakati Ikulu ya Kremlin ikiwa kimya, ndugu wa karibu wa mpinzani namba moja wa Putin, aliyefariki Februari 16 katika jela huko Siberia, wanadai wakabidhiwe mwili wake “mara moja”. Timu ya Alexeï Navalny inadai kuwa hili ni jaribio la "kuficha" mauaji yake.

Picha ya kiongozi wa upinzani wa Urusi Alexei Navalny imewekwa karibu na mishumaa na maua, watu wanapohudhuria hafla ya kutoa heshima kwa kifo cha Navalny, nje ya ubalozi wa Urusi huko Sofia, Bulgaria, Februari 16, 2024.
Picha ya kiongozi wa upinzani wa Urusi Alexei Navalny imewekwa karibu na mishumaa na maua, watu wanapohudhuria hafla ya kutoa heshima kwa kifo cha Navalny, nje ya ubalozi wa Urusi huko Sofia, Bulgaria, Februari 16, 2024. REUTERS - STOYAN NENOV
Matangazo ya kibiashara

 

Timu ya kiongozi wa upinzani nchini Urusi na mkoasoaji mkuuu wa Kremlin Alexeï Navalny aliyeripotiwa kufariki akiwa jela siku ya Ijumaa, inaomba siku ya Jumamosi mwili wake ukabidhiwe familia yake "mara moja", baada ya mamake mwanaharakati huyo kufahamishwa rasmi kuhusu kifo chake gerezani.

"Mfanyakazi katika jela alikokuwa anazuiliwa kiongozi huyo wa upinzani amesema kuwa mwili wa Alexei Navalny ulikuwa Salekhard," mji katika eneo la Urusi la Arctic ambapo alikuwa akizuiliwa, na ulichukuliwa na "wachunguzi" kwa "kufanya 'utafiti'", amebainisha Kira Iarmich, msemaji wa Alexei Navalny.

"Tunaomba mwili wa Alexeï Navalny ukabidhiwe mara moja kwa familia yake," ameongeza, akibainisha kuwa wakuu wa mamlaka ya gereza walimpa mama yake, Lyudmila Navalanïa, hati "rasmi" kuthibitisha kifo cha mwanae.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.