Pata taarifa kuu

Urusi: Serikali yatuhumiwa kwa kuuficha mwili wa Navalny

Nairobi – Watu wa karibu na mwanasiasa wa upinzani nchini Urusi Alexei Navalny wanaishtumu serikali ya Urusi kwa kuuficha mwili wa mpendwa wao, aliyeripotiwa kupoteza maisha akiwa jela hapo jana.

Watu kadhaa wameripotiwa kukamatwa nchini Urusi wakati wakifanya ibaada ya kumkumbuka mwanasiasa huyo wa upinzani
Watu kadhaa wameripotiwa kukamatwa nchini Urusi wakati wakifanya ibaada ya kumkumbuka mwanasiasa huyo wa upinzani AP
Matangazo ya kibiashara

Ndugu wa karibu wa Navalny wamesema, ni wazi kuwa, serikali ya Urusi inagoma kuwapa mwili huo kwa sababu wanajaribu kuficha ushahidi muhimu kuhusu kilichosababisha kifo chake.

Hata hivyo, ripoti zinasema serikali jijini Moscow imesema itakabidhi mwili huo baada ya uchunguzi kukamilika kubaini kilichomuua.

Haijafahamika ni wapi mwili huo, unakohifadhiwa, wakati huu maswali mengi yakiendelea kuulizwa kuhusu mazingira ya kifo cha mpinzani huyo wa rais Vladimir Putin.

Mapema leo, familia ya mwanasiasa huyo, ilithibitisha kutokea kwa kifo cha mpendwa wao na kutaka kukabidhiwa mwili wake, haraka iwezekanvyo.

Kifo cha Navalny, kimelaaniwa na viongozi mbalimbali wa nchi za Magharibi wakiongozwa na rais wa Marekani Joe Biden, ambaye amemshtumu rais Putin kuhusika na kufariki kwa mpinzani wake, aliyekuwa amefungwa jela kwa makosa ambayo yameelezwa kuchochewa kisiasa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.