Pata taarifa kuu

Nchi za Magharibi zanyooshea kidole cha lawama Urusi kwa kifo cha Navalny

Nchi za Magharibi zimeendelea kuweka shinikizo kwa Urusi, zikimshutumu Rais Vladmir Putin na serikali yake kuhusika na kifo cha Alexei Navalny, mkosoaji mkuu wa Rais Vladmir Putin. Wakati huo huo watu wamejitokeza kwa maandamano duniani kote kufuatia kifo cha Alexei Navalny.

Picha kwenye mitandao ya kijamii zilionyesha vikundi vya watu wakiweka maua kwenye makaburi ya muda huko Moscow na Saint Petersburg.
Picha kwenye mitandao ya kijamii zilionyesha vikundi vya watu wakiweka maua kwenye makaburi ya muda huko Moscow na Saint Petersburg. AFP - OLGA MALTSEVA
Matangazo ya kibiashara

 

Kifo cha Alexei Navalny katika gereza la Urusi kimesababisha maandamano na watu wamejitokeza kutoa heshima kwake kote ulimwenguni.

Mashirika ya habari nchini Urusi yanaripoti kwamba jopo la madaktari walijaribu kuokoa maisha ya Navalvy kwa takriban nusu saa lakini ilishindikana kutokana na kile kichotajwa na maafisa wa gereza kuwa "alijihisi vibaya na kupoteza fahamu".

Wafuasi wa mwanaharakati huyo wa kisiasa mwenye umri wa miaka 47 walikusanyika nje ya balozi za Urusi na maeneo mengine katika miji mikubwa duniani kote, ikiwa ni pamoja na London, Paris, Geneva na New York.

Mjini Berlin, umati mkubwa wa watu ulipiga kelele "Putin hadi Hague" na nje ya ubalozi wa Urusi mjini London waandamanaji walishikilia mabango yaliyosema "Navalny ni shujaa wetu".

Mkewe Yulia Navalny ameitaka Jumuiya ya kimataifa kuungana na kuushinda utawala "mbaya na wa kutisha" wa Putin.

Hata hivyo Msemaji wa Kremlin Dmitry Peskov aliwashutumu viongozi wa nchi za Magharibi kwa "mwitikio usiokubalika" juu ya kifo cha Navalny.

Picha kwenye mitandao ya kijamii zilionyesha vikundi vya watu wakiweka maua kwenye makaburi ya muda huko Moscow na Saint Petersburg.

Zaidi ya watu 100 wanaripotiwa kuzuiliwa katika miji mbali mbali ya Urusi.

Rais wa zamani wa Marekani Barack Obama amemtaja Alexei Navalny kuwa "mtetezi asiye na woga wa imani yake ambaye alikufa bila kuvunjwa moyo na ukatili alioupinga".

Obama amesema : "Alipambana na ufisadi, alihamasisha mamilioni ya watu na kamwe hakutetereka katika msisitizo wake wa uhuru wa kujieleza, utawala wa sheria, na Urusi inayowajibika kwa watu na sio dikteta.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.