Pata taarifa kuu

Wanachama wa G7 kuendelea kuisaidia Ukraine katika ulinzi wa angani

Mawaziri wa mambo ya kigeni wa nchi za G7, ambao wamekutana katika kisiwa cha Capri nchini Italia, wameahidi kuendelea kuisaidia nchi ya Ukraine kuimarisha ulinzi wake wa agani.

Mawaziri wa mambo ya kigeni wa nchi za G7 wakati wa kikao chao katika kisiwa cha Capri nchini Italia, April 18, 2024. (Photo by Gregorio Borgia / POOL / AFP)
Mawaziri wa mambo ya kigeni wa nchi za G7 wakati wa kikao chao katika kisiwa cha Capri nchini Italia, April 18, 2024. (Photo by Gregorio Borgia / POOL / AFP) AFP - GREGORIO BORGIA
Matangazo ya kibiashara

Katika taarifa yao, mawaziri hao wameeleza kuwa wanatafuta namna ya kuzitumia mali za Urusi ambazo zimezuiliwa kuisaidia Kyiv.

Viongozi hao wamekutana kuelekea kikao cha wakuu wa nchi za G7 mwezi Juni mwaka huu.

Mawaziri wa mambo ya kigeni wa G7 wameahidi kuendelea kuisaidia Ukraine. Ijumaa, April 19, 2024. (AP Photo/Gregorio Borgia, Pool)
Mawaziri wa mambo ya kigeni wa G7 wameahidi kuendelea kuisaidia Ukraine. Ijumaa, April 19, 2024. (AP Photo/Gregorio Borgia, Pool) AP - Gregorio Borgia

Waziri wa mambo ya kigeni wa Ukraine Dmytro Kuleba ameungana na mwenzake kutoka nchi za Italia, Uingereza, Marekani, Japan,Canada, Ufaransa na Ujerumani kaitka kisiwa cha Capri kwa mazungumzo kuhusu vita kati ya Urusi na Ukraine.

Dmytro Kuleba katika taarifa yake, ametoa wito kwa mataifa mengine kuiiga mfano wa Ujerumani ambayo wikendi iliopita ilitangaza kuwa inatuma mifumo yake ya ulinzi wa agani kwenda nchini Ukraine.

Ukraine imesema inakaribia kuishiwa na silaha za kudungua makombora ya Urusi na ndege zisizo na rubani, hatua inayokuja wakati huu ambapo Urusi imeonekana kuimarisha mashambulio dhidi ya miundombinu ya Kyiv.

Tayari waziri wa mambo ya kigeni wa Ujerumani David Cameron alikuwa amewashinikiza washirika wa G7 kutafuta namna ya kutumia mali za Urusi zilizozuiliwa baada yake kuivamia Ukraine mwaka wa 2022 kuisaidia Kyiv.

 

Hillary Ingati- RFI-Kiswahili /Afp

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.