Urusi: Alexei Navalny mkosoaji wa rais Putin amefariki akiwa jela
Nairobi – Kiongozi mkuu wa upinzani nchini Urusi, Alexei Navalny, amefariki dunia akiwa gerezani, kwa mujibu wa ripoti za maafisa wa Magereza alikokuwa amefungwa.
Imechapishwa:
Ripoti za kutoka kwenye huduma ya magereza zimesema, Navalny alijisikia vibaya ghafla baada ya matembezi siku ya Ijumaa na kupoteza fahamu, na jitihada za kumzindua hazikufua dafu.
Aidha, maafisa nchini Urusi wanasema wanachunguza kufahamu nini kilichomuua mwanasiasa huyo maarufu wa upinzani.
Navalny alifungwa jela miaka 19, tangu mwaka 2021, baada ya kupatikana na makosa ya rushwa na wizi wa Dola Milioni 4.7 zilizokuwa zitumike kwenye mashirika yake ya kisiasa, aliyopinga.
Mwaka uliopita, alihamishiwa kwenye gereza la Arctic, linaloaminiwa kuwa na ulinzi mkali kwenye jimbo la Siberia.
Hata hivyo, mashtaka dhidi ya mwanasiasa huyo, yamekuwa yakiaminiwa kuchochewa kisiasa kwa sababu ya ukosoaji wake kwa rais Vladimir Putin.
Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz amesma Navalny, amelipitia ujasiri wake kupoteza maisha yake, huku Katibu Mkuu wa Jeshi la NATO Jens Stoltenberg akisema kuna maswali mengi kuhusu kifo cha mwanasiasa huyo.
Navalny, aliwahi kuponea kifo bada ya kupewa sumu lakini akatibiwa nchini Ujeurumani na baadaye kuamua kurejea Urusi alipokamatwa jijini Moscow.