Pata taarifa kuu
HAKI-SHERIA

Hukumu ya kifungo dhidi ya Ilya Yashin: Alexei Navalny ashutumu 'hukumu ya aibu'

Licha ya kukamatwa kwake, Ilya Yashin aliendelea kukosoa na kushutumu vitendo vya mamlaka ya Urusi, hata wakati wa kesi yake mwezi Novemba mwaka huu ambapo aliwashutumu majaji wa Urusi kuwa "watumishi" wa mamlaka na kutoa "hisia ya kutokujali kwa Vladimir Putin.

Alexei Navalny kupitia kiungo cha video kutoka chumba anakofungwa katika jela ya IK-2 huko Pokrov, Mei 17, 2022.
Alexei Navalny kupitia kiungo cha video kutoka chumba anakofungwa katika jela ya IK-2 huko Pokrov, Mei 17, 2022. REUTERS - EVGENIA NOVOZHENINA
Matangazo ya kibiashara

Ilia Iachine ambaye alikuwa mshirika wa karibu wa Boris Nemtsov, mpinzani aliyeuawa mnamo 2015 huko Moscow, pia yuko karibu na Alexei Navalny, mpinzani maarufu wa Urusi ambaye pia anazuiliwa jela. Alexei Navalny, adui mkubwa wa Kremlin, ambaye anatumikia kifungo kizito gerezani tangu mwanzoni mwa mwaka wa 2021 baada ya kunusurika kwa sumu, amekashifu hukumu "ya aibu" siku ya Ijumaa katika ujumbe kwenye Instagram.

Kufikia sasa, watu 122 wameshtakiwa kwa "kudharau jeshi". Ni kumi na tano tu ndio wamehukumiwa hadi sasa. Katika kesi kumi, hukumu zilikuwa tofauti: faini, kazi ya lazima au hatua zinazozuia uhuru kama vile kifungo cha nyumbani usiku na kifungo jela; watu watano waliwekwa kizimbani; ni mmoja tu aliyepata kifungo cha miaka saba msimu uliopita wa joto. anashtumiwa: maneno yaliyotolewa Machi 15 mbele ya mkutano wa viongozi wa mitaa waliochaguliwa kutoka wilaya ya Moscow.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.