Pata taarifa kuu

Urusi: Mapato kutokana na mauzo ya mafuta na gesi yapunguwa

Mapato ya mafuta na gesi ya kila mwaka yamepungua kwa 2.1% mnamo mwezi wa  Novemba. Lakini uchunguzi wa karibu wa takwimu rasmi unaonyesha kuwa mapato ya kifedha kutoka kwa bidhaa za nishati yako hatarini, kulingana na vyombo vya habari vya kiuchumi The Bell, ambavyo pia vinajikita kwenye data na uchambuzi kutoka kwa barua inayoheshimiwa juu ya masuala ya kiuchumi na kifedha, MMI.

Mapato ya mafuta na gesi ya kila mwaka yamepungua kwa 2.1% mnamo mwezi Novemba. Lakini uchunguzi wa karibu wa takwimu rasmi unaonyesha kuwa mapato ya kifedha kutoka kwa bidhaa za nishati yako hatarini.
Mapato ya mafuta na gesi ya kila mwaka yamepungua kwa 2.1% mnamo mwezi Novemba. Lakini uchunguzi wa karibu wa takwimu rasmi unaonyesha kuwa mapato ya kifedha kutoka kwa bidhaa za nishati yako hatarini. © Vitaly Nevar / Reuters
Matangazo ya kibiashara

Kwenye karatasi, hakuna kinachobadilika. Pamoja na ruble (fedha za Urusi) bilioni 90 (sawa na euro bilioni 1.3 kwa kiwango cha sasa) zilizokusanywa kutokana na uuzaji wa mafuta na gesi mnamo mwezi wa Novemba, takwimu ziko thabiti kwa bajeti ya serikali ya Urusi. Lakini haya ni matokeo ya uwongo. Kwa mujibu wa vyombo vya habari viwili vya biashara vya Urusi, The Bell na MMI, nusu ya jumla hii ilitokana na malipo yaliyocheleweshwa kutoka kampuni ya Gazprom ambayo ilikuwa ikidaiwa tangu mwaka jana.

Kwa hiyo mapato yamepungua kwa 48.9% kwa mwaka mmoja. Hitimisho: mabadiliko hasi yanaweza kuanzishwa, kulingana na mada mbili maalum. Uzalishaji wenyewe umepungua: – 3.4% ikilinganishwa na mwaka jana. Na uzalishaji wa gesi ulishuka: - 20%.

Kiwango cha juu cha bei ya mafuta nchini Urusi

Hii inatokea wakati vikwazo dhidi ya mafuta ya Urusi havijaanza kutekelezwa: EU, G7 na Australia ziliweka bei kikomo za mafuta Jumatatu Desemba 5, na vile vile vikwazo vya EU juu ya mafuta ya Urusi yanayosafirishwa kwa bahari, miezi kadhaa baada ya marufuku ambayo tayari yameamuliwa na Marekani na Canada.

Kwa vyombo hivi viwili vya habari vya kiuchumi, malengo ya mapato ya bajeti ya Urusi mnamo 2023 hayawezi kufikiwa. Hata hivyo, Urusi ilikuwa tayari inatarajia kushuka kwa kasi kwa mapato yake ya mafuta na gesi. The Bell, inasema hali ya jumla ya bajeti "bado haiwezi kuelezewa kama janga".

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.