Pata taarifa kuu
SIASA-HAKI

Ilya Yashin apewa hukumu nzito kwa kushutumu uvamizi wa Urusi nchini Ukraine

Mmoja wa viongozi wakuu wa mwisho wa upinzani kubaki nchini Urusi amehukumiwa Ijumaa hii, Desemba 9 kifungo cha miaka hadi 8 na nusu jela kwa "kudharau jeshi". Ilia Iachine hadi sasa amehukumiwa kifungo kikali zaidi kwa sababu hii.

Mwanasiasa wa upinzani nchini Urusi Ilia Iachine wakati kesi yake ikisikilizwa mjini Moscow, Desemba 9, 2022.
Mwanasiasa wa upinzani nchini Urusi Ilia Iachine wakati kesi yake ikisikilizwa mjini Moscow, Desemba 9, 2022. REUTERS - POOL
Matangazo ya kibiashara

Ilia Iachine amehukumiwa kifungo cha miaka minane na nusu jela siku ya Ijumaa, kifungo ambacho kilikuwa karibu kulingana na matakwa ya upande wa mashtaka, uliotaka kifungo cha miaka tisa jela. Anahukumiwa kwa kushutumu, wakati wa mahojiano yake ya moja kwa moja kwenye mtandao wa YouTube "mauaji ya raia" katika jiji la Ukraine la Bucha, moja ya vitongoji vya mji wa Kyiv, ambapo jeshi la Urusi lilishutumiwa kwa mauaji ya kikatili wakati likishikilia  eneo hili, madai ambayo Moscow inakanusha.

Ilia Yachin, mpinzani mashuhuri wa Vladimir Putin, mwenye umri wa miaka 39, alikamatwa mnamo mwezi Juni mwaka jana kwa kueneza 'habari za uwongo' kuhusu vitendo vya jeshi la Urusi nchini Ukraine, na pia kwa 'uchochezi wa chuki'. Uhalifu unaoadhibiwa kwa miaka kumi gerezani nchini Urusi kwa misingi ya Kanuni ya Adhabu ambayo ilianzishwa muda mfupi baada ya kuanza kwa mashambulizi ya Urusi nchini Ukraine na ambayo inawaadhibu wale 'wanaodharau' jeshi la Urusi au "kuchapisha habari za uongo" kuhusu matendo yake.

Ilia Yachin amekaribisha uamuzi huo kwa kicheko, huku wafuasi wake wakilia kwa hasira katika chumba cha mahakama, linaripoti shirika la habari la AFP. Kesi yake ilitazamwa hasa nchini Urusi, kwani alikuwa mmoja wa wapinzani mashuhuri wa mwisho wa Urusi ambaye hakuikimbia nchi yake au kufungwa. "Miaka minane na miezi sita jela... wahusika wa hukumu hii wana matumaini kuhusu matarajio ya Vladimir Putin," amejibu. Kwa maoni yangu, nina matumaini sana. Nguvu utawala unataka kututisha sisi sote, lakini kwa kweli unaonyesha udhaifu wake tu. Siogopi na haupaswi kuogopa. Mabadiliko yanakaribia haraka. "

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.