Pata taarifa kuu

Alexei Navalny atunukiwa Tuzo ya Bunge la Ulaya Sakharov

Mwaka huu Bunge la Ulaya limemtunuku Tuzo maalum ya Haki za Binadamu ya Sakharovkiongozi wa upinzani nchini Urusi Alexeï Navalny, aambaye anazuiliwa nchini mwake.

Mpinzani wa Urusi Alexei Navalny kwa sasa amezuiliwa katika kambi ya jeshi huko Siberia.
Mpinzani wa Urusi Alexei Navalny kwa sasa amezuiliwa katika kambi ya jeshi huko Siberia. Vasily MAXIMOV AFP/File
Matangazo ya kibiashara

Alexei Navalny anazuiliwa jela tangu aliporejea nchini Urusi mwezi Januari mwaka jana katika katika jela lililo chini ya ulinzi mkali, kilometa 100 mashariki mwa Moscow, anatumikia kifungo cha miaka miwili na nusu.

Mnamo Agosti iliyopita, mpinzani wa Urusi alizungumza na Gazeti la New York Times na kuelezea mazingira ya kuzuiliwa kwake, chini ya mpango uliotengenezwa na mamlaka: kutazama filamu za runinga za serikali ya Urusi na filamu za propaganda kwa zaidi ya saa nane kwa siku. Kusoma, kuandika au shughuli nyingine yoyote amepigwa marufuku.

Alexeï Navalny, wakili wa zamani mwenye umri wa miaka 45, amekuwa mkosoaji mkuu wa Vladimir Putin. Kwa miaka mingi, amelaani ufisadi nchini Urusi, akilenga viongozi serikalini, wabunge na mawaziri, kupitia video zilizochapishwa kwenye mitandao ya kijamii.

Mnamo Agosti 2020, alipewa sumu huko Tomsk, Siberia. Moscow imekanusha kuhusika kwa jambo hilo. Navalny alifungwa gerezani aliporudi nchini Urusi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.