Pata taarifa kuu

Urusi yaharibu ndege zisizo na rubani za Ukraine katika mji wa Moscow na Bahari Nyeusi

Urusi imetangaza leo Ijumaa kuwa imeharibu ndege zisizo na rubani za Ukraine huko Moscow na katika Bahari Nyeusi, maeneo mawili ambapo mashambulizi hayo yameongezeka katika wiki za hivi karibuni katika muktadha wa mashambulizi ya Ukraine na kujiondoa kwa Moscow kwenye makubaliano ya nafaka katikati ya mwezi wa Julai.  Fuata saa baada ya saa matukio ya hivi punde kuhusu vita nchini Ukraine.

Meli zilizolengwa, kulingana na Moscow, "zilikuwa zikifanya kazi za udhibiti katika sehemu ya kusini-magharibi ya Bahari Nyeusi, kilomita 237 kusini magharibi mwa Sevastopol", makao makuu ya jeshi la wanamaji la Urusi.
Meli zilizolengwa, kulingana na Moscow, "zilikuwa zikifanya kazi za udhibiti katika sehemu ya kusini-magharibi ya Bahari Nyeusi, kilomita 237 kusini magharibi mwa Sevastopol", makao makuu ya jeshi la wanamaji la Urusi. (Photo : C. Magnard/RFI)
Matangazo ya kibiashara

Mfumo wa Ulinzi wa anga wa Urusi umeharibu ndege isiyo na rubani huko Moscow ambayo haikusababisha uharibifu au majeruhi, meya wa mji mkuu wa Urusi amesema mapema Ijumaa. "Jana usiku, wakati wa jaribio la kufika Moscow, vikosi vya ulinzi wa anga viliharibu ndege isiyo na rubani. Mabaki ya ndege hiyo yalianguka kwenye eneo la Kituo cha Maonyesho, na hayakusababisha uharibifu mkubwa kwa jengo hilo ", amesema Sergei Sobyanin, ambaye ameongeza kuwa hakukuwa na waathiriwa kulingana na habari ya kwanza.

Wakati huo huo Urusi imesema ilizuia Alhamisi jioni shambulio la Ukraine lililotekelezwa na ndege isiyo na rubani dhidi ya meli zake zilizopo katika Bahari Nyeusi, ambapo mapigano yameongezeka tangu kujiondoa kwa Moscow katika makubaliano ya nafaka katikati ya mwezi wa Julai.

Meli zilizolengwa, kulingana na Moscow, "zilikuwa zikifanya kazi za udhibiti katika sehemu ya kusini-magharibi ya Bahari Nyeusi, kilomita 237 kusini magharibi mwa Sevastopol", makao makuu ya jeshi la wanamaji la Urusi.

(Pamoja na AFP na Reuters)

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.