Pata taarifa kuu

Mashambulizi ya Urusi yaua sita kusini mwa Ukraine

Watu sita wameuawa, ikiwa ni pamoja na mtoto mchanga, wakati wa mashambulizi ya Urusi siku ya Jumapili kwenye eneo la Kherson, kusini mwa Ukraine, serikali ya Kiev imetangaza.

Hivi karibuni Wizara ya ulinzi ya Urusi ilisema kuwa vikosi vyake vimeharibu ndege 20 zisizo na rubani za Ukraine kwenye rasi ya Crimea inayokaliwa na Urusi.
Hivi karibuni Wizara ya ulinzi ya Urusi ilisema kuwa vikosi vyake vimeharibu ndege 20 zisizo na rubani za Ukraine kwenye rasi ya Crimea inayokaliwa na Urusi. via REUTERS - STATE EMERGENCY SERVICE OF UKRAI
Matangazo ya kibiashara

"Urusi imeua watu sita katika eneo la Kherson," Waziri wa Mambo ya Ndani wa Ukraine Igor Klymenko amesema. Shambulio hilo limesababisha vifo vya watu wazima watatu na mtoto mchanga wa siku 23 katika eneo la Shyroka Balka na watu wengine wawili katika eneo la Stanislav.

Hivi karibuni Wizara ya ulinzi ya Urusi ilisema kuwa vikosi vyake vimeharibu ndege 20 zisizo na rubani za Ukraine kwenye rasi ya Crimea inayokaliwa na Urusi.

Ndege kumi na nne zisizo na rubani ziliharibiwa na mifumo ya ulinzi wa anga na sita ziliharibiwa kupitia mfumo wa  kielektroniki kwa mujibu wa wizara hiyo.

Sergei Kryuchkov, mshauri wa gavana wa Crimea aliyewekwa na Urusi, alisema hapo awali kuwa mifumo ya ulinzi wa anga ilizima mashambulio ya anga katika maeneo tofauti.

Siku ya Ijumaa, maafisa wa Urusi walisema kwamba ndege zisizo na rubani za Ukraine zilidunguliwa zilipokuwa zikijaribu kushambulia Moscow - siku ya tatu mfululizo ya majaribio ya kushambulia mji mkuu wa Urusi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.