Pata taarifa kuu

Saudi Arabia: Mazungumzo kuhusu Ukraine kufanyika, lakini na nani?

Saudi Arabia inaandaa mazungumzo kuhusu Ukraine wikendi hii. Takriban nchi thelathini zimealikwa, Urusi haitashiriki mazungumzo haya. Huu ni mkutano wa pili wa aina hii tangu ule wa Copenhagen mwezi Juni mwaka jana.

Mwanamfalme wa Saudia Mohammed bin Salman huko Jeddah mnamo Julai 19, 2023.
Mwanamfalme wa Saudia Mohammed bin Salman huko Jeddah mnamo Julai 19, 2023. AFP - -
Matangazo ya kibiashara

Mamlaka nchini Saudi Arabia imefanya siri mazungumzo haya. Lakini kulingana na vyanzo kadhaa, majadiliano yalifanyika Jeddah, kwenye mwambao wa Bahari ya Shamu, ambapo nchi kadhaa za kusini kama vile Brazil au India, ambazo hazijaegemea upande wowote katika mzozo kati ya Urusi na Ukraine, zinapaswa kushiriki.

Marekani na Umoja wa Ulaya zitawakilishwa, lakini si katika ngazi ya juu. china, mhusika mkuu katika mzozo huu, haijajulikana kama itashiriki au la katika mazungumzo haya. Vyombo vya habari vya China vinatangaza kuwa Beijing itawakilishwa na Li Hui, mwakilishi maalum wa serikali ya China katika Masuala ya Eurasia. Urusi haitahudhuria.

Kwa mujibu wa rais wa Ukraine, ambaye alizungumza na wanadiplomasia wa nchi yake Jumatano wiki hii, mkutano huu unapaswa kufanya iwezekane kuandaa mkutano wa kilele wa amani nchini Ukraine ambao unaweza kufanyika msimu ujao. Volodymyr Zelensky alitumia fursa hii kukumbusha msimamo wa nchi yake kuhusu uwezekano wa mazungumzo ya amani.

Mpango wake wa amani wenye vipengele kumi, uliowasilishwa na rais wa Ukraine kwenye Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mnamo mwezi Septemba 2022, ulifafanuliwa katika kikoa cha kundi la G20 nchini Indonesia miezi miwili baadaye. Hasa, hutoa urejesho kamili wa uadilifu wa eneo la Ukraine, ikiwemo Crimea, pamoja na kuondoka kwa askari wa Urusi.

Moscow haizingatii hata kidogo kuondoa wanajeshi wake katika ardhi ya Ukraine, kama rais wa Urusi alivyokumbusha siku chache zilizopita. Kwa mujibu wa Vladimir Putin, masuala pekee yanayoweza kujadiliwa ni kumeguliwa 20% ya nchi ya Ukraine, ambayo ni kusema Donbass na Crimea.

Kwa hivyo maendeleo yoyote yanaonekana kuwa magumu, au hayawezekani, kwa sasa. Mazungumzo haya hata hivyo yanapaswa kuiwezesha Saudi Arabia kujiweka kama mpatanishi katika mzozo huo. Riyadh ina nafasi ya kuzungumza na pande zote mbili, Ukraine na Urusi. Kwa kujaribu kuonyesha kuwa inatetea amani, mamlaka ya Saudia pia inatumai kufuta taswira yao mbaya ya haki za binadamu.

Chochote kitakachotokea, ni ushindi wa kidiplomasia kwa Mwanamfalme Mohammed bin Salman. Hii inafafanuliwa na mtafiti Sébastien Boussois.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.