Pata taarifa kuu

Urusi yadai kudungua ndege 13 zisizo na rubani za Ukraine karibu na Crimea na Moscow

Wizara ya Ulinzi ya Urusi imedai mapema Alhamisi kwamba imedungua ndege 13 zisizo na rubani, zikiwemo 11 karibu na Crimea na mbili zikielekea Moscow, baada ya mashambulizi kadhaa sawia katika siku za hivi karibuni. Fuata matukio ya hivi punde katika vita vya Ukraine.

Wizara ya Ulinzi ya Urusi imedai mapema Alhamisi kwamba imedungua ndege 13 zisizo na rubani, zikiwemo 11 karibu na Crimea na mbili zikielekea Moscow.
Wizara ya Ulinzi ya Urusi imedai mapema Alhamisi kwamba imedungua ndege 13 zisizo na rubani, zikiwemo 11 karibu na Crimea na mbili zikielekea Moscow. © Alexander Nemenov, AFP
Matangazo ya kibiashara

"Ndege mbili zisizo na rubani zilizokuwa zikiruka kuelekea mji wa Moscow zimeharibiwa," Wizara ya Ulinzi ya Urusi imesema kwenye Telegram. Kombora moja lililolenga mji mkuu wa Urusi lilidunguliwa na mfumo wa ulinzi wa anga wa Urusi katika mkoa wa Kaluga, kusini magharibi mwa mji mkuu, mji wa pili kwa ukubwa katika wilaya ya Odintsovo, katika mkoa wa Moscow, wizara imeripoti, ikiishutumu Kiev kwa kurusha ndege hizo.

"Karibu na mji wa Sevastopol, huko Crimea, ndege mbili zisizo na rubani zimepigwa na vifaa vya mfumo wa ulinzi wa anga, zingine tisa ziliangushwa kwa njia za kivita za kielektroniki na kuanguka kwenye Bahari Nyeusi kabla ya kufikia malengo yao. Hakuna majeruhi au uharibifu ulioripotiwa, wizara imesema.

Pamoja na AFP na Reuters

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.